Wana Yanga hii inawahusu

Mohamed Mbelwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
507
Reaction score
272
Anaandika Emmanuel M. Makalla mmoja kati ya wanachama wachache wa Yanga wenye akili timamu.
______
Natafuta tusi moja niwatukane viongozi wa Yanga lakini najikuta roho mtakatifu ameficha maneno yote machafu.

Hivi hapo Yanga hakuna watu wa masoko wawafundishe nini maana ya nembo ya biashara?

Hivi Mwakalebela bado una mambo ya kitoto hivyo kiasi kwamba hadi unaona nembo ya Vodacom inabadilisha rangi ya jezi za Yanga?

Na wewe Dr. Mshindo Msolla hivi ukiamka kesho asubuhi ukakuta nembo ya CAF imebadilishwa na kuwa na rangi NYEUPE na Yanga ikaingia hatua ya makundi michuano ya CAF mtagomea nembo hiyo ya CAF yenye rangi nyeupe?

Kwa huu ujinga wenu bora tufungwe tu Zesco United....pengine akili zitawakaa sawa... utoto kabisa.

Hivi hii ndio Yanga mpya mlioitangaza? Hivi kwa huu upuuzi tunaweza kuwatofautisha vipi na mzee Akilimali?

Mwambieni Zahera awe anavaa t-shirt za njano na kijani pekee akiwa kazini maana kuna wakati anavaa hadi zenye rangi ya blue wakati sio utamaduni wa Yanga na katiba inakataza.

TFF msimu huu nawaaminia kwa misimamo kazeni hivyo hivyo na msiwape nafasi ya kugomea udhamini wa Vodacom maana hawa watu jeuri sana au washushwe daraja kabisa.

Kuna shida gani hiyo nembo nyekundu ya Vodacom kukaa begani? Kwani itakuwa imebadilisha rangi ya jezi?

Ujinga ujinga ujinga.!
 
Huyo mtu hawezi kuwa Yanga
 
TFF na VODACOM hawana ubavu wa kushindana na Yanga, timu ya wananchi, timu iliyopigania uhuru wa TAIFA
Vodacom sio machizi. Wanaijua nguvu ya Yanga.

Nadhani busara ya watu wa Vodacom imetumika na Yanga haitavaa doa jekundu.

Halafu tu wepesi wa kusahau. Miaka ya nyuma chini ya udhamini wao, Yanga ilitumia ua jeusi.

Msomali Karia alitaka kutikisa kiberiti cha Yanga. Amekuta njiti zimejaa tele. Akawaambie mabwana zake wa Mikia kwamba Yanga si ya kuchezea.

Vodacom wameona mbali sana. Yanga ingeweza kuingia mkataba na kampuni nyingine ya simu. Pangechimbika.
 
Mi nilijua hilo tangia mwanzo.Halafu watu wanapotosha kuwa nembo ya vodacom ni nyekundu tu.wkati kuna nembo ile nyeupe na kuna nyekundu.nadhani voda wametumia busara maana hii ingeleta mgogoro usio na maana wakati wao wana rangi nyingi.
 
kama mnaamini katiba yenu nendeni mkaanzishe ligi yenu ukooooo, acheni kuharibu Biashara ya Mtu.
 
Miaka ya nyuma tulikataa na Voda wakatuwekea nyeusi iweje leo iwe Ngumu? Ile ni précédent inabind hata kwa kanisa ni ya promissory estopell
 
Inashushwa daraja
 
Naunga mkono hoja badala ya kujadili mambo ya msingi wanajadili nembo ndio manana tunafungwa had na pamba inasikitisha Sana Msola fukuza huyo Zahera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…