Mohamed Mbelwa
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 507
- 272
Anaandika Emmanuel M. Makalla mmoja kati ya wanachama wachache wa Yanga wenye akili timamu.
______
Natafuta tusi moja niwatukane viongozi wa Yanga lakini najikuta roho mtakatifu ameficha maneno yote machafu.
Hivi hapo Yanga hakuna watu wa masoko wawafundishe nini maana ya nembo ya biashara?
Hivi Mwakalebela bado una mambo ya kitoto hivyo kiasi kwamba hadi unaona nembo ya Vodacom inabadilisha rangi ya jezi za Yanga?
Na wewe Dr. Mshindo Msolla hivi ukiamka kesho asubuhi ukakuta nembo ya CAF imebadilishwa na kuwa na rangi NYEUPE na Yanga ikaingia hatua ya makundi michuano ya CAF mtagomea nembo hiyo ya CAF yenye rangi nyeupe?
Kwa huu ujinga wenu bora tufungwe tu Zesco United....pengine akili zitawakaa sawa... utoto kabisa.
Hivi hii ndio Yanga mpya mlioitangaza? Hivi kwa huu upuuzi tunaweza kuwatofautisha vipi na mzee Akilimali?
Mwambieni Zahera awe anavaa t-shirt za njano na kijani pekee akiwa kazini maana kuna wakati anavaa hadi zenye rangi ya blue wakati sio utamaduni wa Yanga na katiba inakataza.
TFF msimu huu nawaaminia kwa misimamo kazeni hivyo hivyo na msiwape nafasi ya kugomea udhamini wa Vodacom maana hawa watu jeuri sana au washushwe daraja kabisa.
Kuna shida gani hiyo nembo nyekundu ya Vodacom kukaa begani? Kwani itakuwa imebadilisha rangi ya jezi?
Ujinga ujinga ujinga.!