Miaka ya nyuma tulikataa na Voda wakatuwekea nyeusi iweje leo iwe Ngumu? Ile ni précédent inabind hata kwa kanuni ya promissory estopell
Sisi hatuna neno mtani tuko very professional si unaona Logo ya CAF tuliivaa ya kijani kabisa.Nasikia yameshaisha eti Mtani. Ila nawaza tu ingekuwa nyie mngekubali?
Hizi nikauli zenu Mtani.Sisi hatuna neno mtani tuko very professional si unaona Logo ya CAF tuliivaa ya kijani kabisa.
.
Ninyi uswahili mwingi
Hivi mtani Timu zote za VPL mfano Azam fc, Kagera sugar, Mtibwa Sugar, Mbao fc, Singida united, Alliance fc, Mwadui fc, JKT Ruvu na wenzao wasiovaa jezi nyekundu ukiwaacha Coastal union n.kHizi nikauli zenu Mtani.
Ila niseme tu hao Vodacom wana lao jambo sababu sio kwamba ndio wanaanza kuidhamini TPL kwa mara ya kwanza.
Hii nyekundu wangeileta tangia mwanzo hapo sawa sasa umruhusu msimu huu avae nyeusi kisha mbeleni ulazimishe avae nyekundu huoni wanataka kuleta mkanganyiko.
Eti umesema huyo mwandishi ana akili timamu?Kitokee nini hadi mwanachama mwenye akili timamu aitakie timu yake laana ya kushuka Daraja? Huyo ama si mwanachama wa timu anayoitakia ishuke daraja, au hana akili timamu, au yote mawili kwa pamoja.Anaandika Emmanuel M. Makalla mmoja kati ya wanachama wachache wa Yanga wenye akili timamu.
______
Natafuta tusi moja niwatukane viongozi wa Yanga lakini najikuta roho mtakatifu ameficha maneno yote machafu.
Hivi hapo Yanga hakuna watu wa masoko wawafundishe nini maana ya nembo ya biashara?
Hivi Mwakalebela bado una mambo ya kitoto hivyo kiasi kwamba hadi unaona nembo ya Vodacom inabadilisha rangi ya jezi za Yanga?
Na wewe Dr. Mshindo Msolla hivi ukiamka kesho asubuhi ukakuta nembo ya CAF imebadilishwa na kuwa na rangi NYEUPE na Yanga ikaingia hatua ya makundi michuano ya CAF mtagomea nembo hiyo ya CAF yenye rangi nyeupe?
Kwa huu ujinga wenu bora tufungwe tu Zesco United....pengine akili zitawakaa sawa... utoto kabisa.
Hivi hii ndio Yanga mpya mlioitangaza? Hivi kwa huu upuuzi tunaweza kuwatofautisha vipi na mzee Akilimali?
Mwambieni Zahera awe anavaa t-shirt za njano na kijani pekee akiwa kazini maana kuna wakati anavaa hadi zenye rangi ya blue wakati sio utamaduni wa Yanga na katiba inakataza.
TFF msimu huu nawaaminia kwa misimamo kazeni hivyo hivyo na msiwape nafasi ya kugomea udhamini wa Vodacom maana hawa watu jeuri sana au washushwe daraja kabisa.
Kuna shida gani hiyo nembo nyekundu ya Vodacom kukaa begani? Kwani itakuwa imebadilisha rangi ya jezi?
Ujinga ujinga ujinga.!
Yanga sio mambumbumbu
Upi?Huo ni uganga wa kienyeji
Bahati mbaya hamchezi ligi yenu, hivyo inabidi mfuate masharti ya wale mnaocheza ligi yaoYanga hatutavaa hiyo nembo nyekundu hiyo ni kinyume cha katiba yetu,