WANA-YANGA KARIBUNI, WATANI ZETU MTUSAIDIE MAWAZO.

WANA-YANGA KARIBUNI, WATANI ZETU MTUSAIDIE MAWAZO.

chaliko

Senior Member
Joined
Apr 1, 2019
Posts
180
Reaction score
803
Naomba niwasalimu wana JF wote.

Nasikitika kuona Yanga wakichangishana Mara kwa Mara ili kupata FEDHA ya kuendeshea timu.

Naomba nilete njia mbadala ya kuondokana na hali hii kwa WANAYANGA.

Naomba nitoe Somo kidogo kwa YANGA.

i.Yanga inahitaji kubadili mfumo wa uongozi na uendeshaji timu.

a) Iwe na matawi ya kudumu Mikoani na Wilayani.

b) Iruhusu hata Wanachama wa Mikoani na Wilayani kumiliki kadi na kuchagua Viongozi wao. Hii itasaidia Wanachama wa Mikoani kuona kuwa Yanga ni timu yao na pia kuwa na Viongozi Imara.

NAMNA GANI WANACHAMA WA MIKOANI WATACHAGUA VIONGOZI WAO.

i.Wagombea wote watambuliwe na Wanachama kwa kila Mkoa na Wilaya.

ii.Siku ya Uchaguzi Kamati itume au itumie Mawakala maalumu wa kusimamia uchaguzi kwa kila Mkoa na Wilaya. Mawakala hawa watahakikisha Kanuni zinazingatiwa.

iii.Uchaguzi ufanyike kwa wakati mmoja Nchi mzima na Mshindi atangazwe baada ya kukusanya na Kuhesabu KURA za Nchi nzima kwenye Matawi husika.

c). Sifa ya mpiga kura.
i.Awe na akili timamu
ii.Awe amelipa ADA yake yote. (Asiwe anadaiwa)
iii.n.k

d). MFUMO WA ADA.
i.Kila Mwanachama atatakiwa kulipa ADA ya Tshs 500/= au 1,000/= Kwa Mwezi kwa Mwanachama Mmoja


ii.Jumla ya ADA kwa Mwaka itakuwa Tshs 6,000/= au Tshs 12,000/= kwa Mwanachama mmoja.

KIASI HIKI KINATOSHA KABISA KUENDESHA TIMU KWA ANGALAU 75%-80% au hata 100%.

Kama itabaki 25%-20% INAWEZA KUTUMIKA FEDHA YA WADHAMINI WA LIGI AU TIMU.


HESABU FIKIRISHI.

Kama Yanga ina Wanachama 6,000,000 Tanzania nzima.

a) 500/= x 600,000 = 300,000,000/= Kwa Mwezi

AU

b) 1,000/= x 600,000 = 600,000,000/= Kwa Mwezi

NB:
1. Yanga ikiwa na Wanachama 1,000,000 au 2,000,000 au 3,000,000 au 4,000,000 au 5,000,000 Je ni Kiasi gani watakusanya?

2. JE FEDHA HIZI HAZITOSHI KUENDESHA TIMU KWA MWEZI?


Nawasilisha.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna tofauti na wanaolima matikiti kupitia wasapu groups.

Cha kushangaza utakuta mtu mwenye kudhani ana mawazo mapana hata pesa ya kula tu inamsumbuwa.
 
YANGA KIKUNDI CHA USHANGILIAJI CHA WAGENI NACHO KINAHITAJI MAHESABU YOTE HAYO? SASA itakuwa taabu hapa mjini, hela zote hizo kushangilia tuuuuu
 
Mkuu fikirikwanza,

Hapa nimechambua Wanachama na siyo Mashabiki.

Mwanachama ni yule mwenye kadi ambayo analazimika kuilipia kila Mwaka lakini Shabiki hana kadi.

Kuna watu wapo hapa Tanzania na ni Watanzania lakini wana kadi za uanachama wa timu za uingereza na wanalipa ada kila Mwaka.

ADA NI CHANZO CHA MAPATO.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu Matola,

Ni sawa ila MTAJI wa Kwanza ambao unatakiwa kuwa nao Mwanadamu ni FIKRA CHANYA. Pesa na vingine hufuata.

Hapa Mimi nimeweka fikra zangu ambazo naamini ni Chanya.

Huna tofauti na wanaolima matikiti kupitia wasapu groups.

Cha kushangaza utakuta mtu mwenye kudhani ana mawazo mapana hata pesa ya kula tu inamsumbuwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom