Wana Yanga msikate tamaa

Wana Yanga msikate tamaa

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Mwezi wa 6 mwaka huu nilisema ni lazima Yanga atafika mbali kimataifa. Na siogopi kusema hivyo. Nilisema Yanga mechi za nyumbani atakuwa anafanya vibaya ila akifika ugenini ndiyo moto unatawaka.

Subiri sasa kwenye mechi ya marudiano kule Sudan, kuna watu watajiuliza imewezekanaje?

Ngoja tuone,

Ila tafuteni mabeki wazuri!
 
Bado wana nafasi ya kusawazisha makosa yao japo kiuhalisia ni ndogo sana.

Hata wewe haijalishi ni shabiki wa Yanga kiasi gani ila kama uko serious unabeti ili upate hela huwezi kuibetia Yanga ipate matokeo huko away.

Unajua hii mechi ingekuwa rahisi kubashiri Yanga kupata matokeo ugenini endapo Al Hilal leo tungeona wana zuia

Lakini mechi ambayo Diarra ndio man of the match basi huko away itakuwa ni zaidi ya hapa.

Na huko Confederation nako mambo ni magumu, kuna timu zimechafukwa zinashusha vipigo balaaa.

Huyo Azam kapasuka bao 3, unaweza ukafikiria kuwa una nafasi ya kusawazisha makosa yako pindi ukiangukia Confederation lakini unagudua walioko Confederation nao washatolewa wanataka wakasawazishe makosa yao NBC
 
watafute mabeki wazuri wapi? wanawatafutia wapi?
 
Hivi unajua kweli unachoongea wewe!?????[emoji23][emoji23][emoji23]unaongea kiutani ila yule ibenge ana roho mbaya sana,na kule sudan wakipata hata shoot on target sijui
 
Siumii yanga kufungwa. Siumii yanga kutolewa. Kinachoniuma ni wachezaji kuwa wapumbavu. Haiwezekani mtu amewekeza maisha yake yote kwenye club alafu wachezaji wanafanya upumbavu. Ni nini hao wachezaji wanakosa saivi!?? Kmmke
 
Mwezi wa 6 mwaka huu nilisema ni lazima Yanga atafika mbali kimataifa. Na siogopi kusema hivyo. Nilisema Yanga mechi za nyumbani atakuwa anafanya vibaya ila akifika ugenini ndiyo moto unatawaka....
Wakati unaiongelea Yanga, timu yako inayocheza leo imeshafuzu hatua ya makundi? Au mnafikiri mpira unachezwa mdomoni kama mlivyo zoea?

Yaani mnavyo ijadili Yanga, unaweza kufikiri labda kwa upande wenu mlishafuzu tayari hatua ya makundi! Nyinyi ndiyo maana huwa tunawafunga kila mechi.napenda sana kucheza mpira mdomoni, badala ya uwanjani.
 
Mwakajana Manara aliyaita mashindano ya CAF Confederation kama kombe la loosers baada ya Simba kuangukia huko ...sasa nasubiri mwakahuu utoporoo mkishatolewa Sudan mtayaitaje hayo mashindano🤣🤣🤣
 
Mwakajana Manara aliyaita mashindano ya CAF Confederation kama kombe la loosers baada ya Simba kuangukia huko ...sasa nasubiri mwakahuu utoporoo mkishatolewa Sudan mtayaitaje hayo mashindano🤣🤣🤣
Kwa hiyo nyinyi mna uhakika mtaingia makundi siyo, na hiki kikosi chenu cha tia maji tia maji! Yaani timu inategemea hamasa kutoka kwa Juma Mgunda!! Halafu ifuzu, na Yanga iliyokamilika kila idara, ishindwe!!

Haya yatakuwa ni maajabu.
 
Simba ni simba tu mra. Subiri tu uingie CAFcc huko nako ukapigwe kama ngoma urudi nyumbani kujipigia vitoto vyako vya NBC PL ulivyovizoea.

Mashindano ya wakubwa uto hawezi labda apewe timu ya vipofu

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Wakati unaiongelea Yanga, timu yako inayocheza leo imeshafuzu hatua ya makundi? Au mnafikiri mpira unachezwa mdomoni kama mlivyo zoea?

Yaani mnavyo ijadili Yanga, unaweza kufikiri labda kwa upande wenu mlishafuzu tayari hatua ya makundi! Nyinyi ndiyo maana huwa tunawafunga kila mechi.napenda sana kucheza mpira mdomoni, badala ya uwanjani.
Mpaka sasa haujasikia tambo zozote kutoka kwa viongozi na mashabiki wa Simba Sc kuwa wataipasua De Agosto, ila hali ilikuwa tofauti kwenu mlipoidharau Hilal na kudai kuwa mtaipiga kama ngoma.

Kwahiyo nyinyi ndo mlidhani mpira unachezewa mdomoni sio sisi, sisi tumewaheshimu wapinzani wetu.
 
Kwa hiyo nyinyi mna uhakika mtaingia makundi siyo, na hiki kikosi chenu cha tia maji tia maji! Yaani timu inategemea hamasa kutoka kwa Juma Mgunda!! Halafu ifuzu, na Yanga iliyokamilika kila idara, ishindwe!!

Haya yatakuwa ni maajabu.
Unaiona timu yako imekamilika kwa sababu ya vihongo hongo mnavyotoa kwa wapinzani.
Ila ina mapungufu mengi na inafungika kirahisi.

Nakubali tu kuwa mna washambuliaji bora kwa sasa.Ila hamna beki.
 
Back
Top Bottom