Wana Yanga SC tugomeni GSM watuachie Timu yetu wakikataa tuhamieni rasmi Simba SC kwenye raha kwani tumechoka sasa!

Wana Yanga SC tugomeni GSM watuachie Timu yetu wakikataa tuhamieni rasmi Simba SC kwenye raha kwani tumechoka sasa!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Hivi kweli wana Yanga SC kulikuwa na Umuhimu wowote wa Kuachana na Kocha Mwambusi na kutuletea hawa Wala Tende wa Tunisia Nabi na Wenzake?

Hivi kweli GSM ni wa Kutusajilia Yanga SC yetu hii Migalasa akina Sarpong, Yacoiba, Fiston na Ntibanzonkiza ambaye sioni hata nini anafanya Uwanjani zaidi ya Kurukaruka tu hovyo Uwanjani kama Maharage ya Kyela.

Hivi kweli Injinia Hersi ni wa Kutudanganya kabisa Sisi wana Yanga SC tena na Kutuaminisha kabisa kuwa Yanga SC tunakuwa Mabingwa wa VPL Msimu na kwamba tusipokuwa Mabingwa aulizwe Yeye?

Hivi kweli Wana Yanga SC Kipa Farouk Shikalo ni wa Kuidakia Yanga SC yetu huku tukimtenga Kipa Bora tuliyenae na aliyetuokoa Metacha Mnata kwakuwa tu amehusishwa kutaka kujiunga na Simba SC?

Hivi kweli wana Yanga SC Leo hii pamoja na Umasikini Wetu GSM na Uongozi unaweza kuacha Kuiandaa Timu kwa ajili ya Mechi ya Leo na Wote kukimbilia Mwanza ili Kuidhoofisha Simba SC isishinde wakati tayari imeshakomba Alama zote Tisa ( Kenda ) kutoka Kanda ya Ziwa?

Wana Yanga SC kama mpaka Kesho hatujakutana Klabuni ili GSM na Yanga SC watuachie Timu yetu Mimi nitahamia rasmi Simba SC kwani huko ndiko kwenye Raha, Amani na Furaha ambako nahisi naweza hata Kunenepa baada ya Kukondeshwa sana na Yanga SC hii ya sasa.
 
Nafasi Ya Kushiriki michuano Kimataifa ya kubebwa na Simba iwapo itatokea pia MGOMO UENDELEEEE......!
 
Back
Top Bottom