Wana Yanga SC tukutane hapa ili tuanze Kutengeneza na Kubuni mapema sababu ya Kipigo tutakachokipata leo huko Botswana

Ndiyo maana naipenda Yanga SC yangu. Aliyesema Yanga SC havuki nani? Haya sasa Yanga SC ndiyo tumevuka hivyo tunamngojea ajae hata kama wakiwa ni wanaojua Mpira Simba SC nao waje tu. Chezea Balinya na Sibomana Wewe? Kuanzia leo Mechi zote Yanga SC itashinda na tunaenda kuwa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho hili na kwa Yanga SC hii ya leo hata wakija Liverpool au Barcelona au PSG au AC Millan wanapigwa tu. Leo nina amani mno kwa Ushindi huu wa Timu yangu pendwa kabisa ya Yanga SC. Na nawaombeni sasa Viongozi wangu wa Yanga SC acheni ule mpango wenu wa Kumuondoa Kocha Zahera na Msaidizi wake Mwandila ili mumlete huyo Mserbia wenu na asaidiwe na Ambani sijui Mwalala kutoka Kenya. Kama kweli Yanga SC tunataka Kocha mzuri basi ni kheri tuwaombe Simba SC watuazime Makocha wao kwani watatupeleka mbali mno.
 
Yani mbumbumbu bhana unaandika kwa machungu na aibu.Aibu na kudharauliwa milele.Hii ndo Yanga Tunapindua mez kibabeeee.
 
zimia sasa
 
Mimi ni mwana simba kindaki ndaki lakini linapokuja swala la timu zetu kuwakilisha nchi nauvua usimba na kuwaunga mkono wale wote wanao wakilisha nchi.

Nimefurai sana matokeo aliyoyapata mtani wangu kanda 2 nawapongeza wana kwasu kwasu wote kwa ushindi wa leo ni heshima kwa taifa letu.

kwa wale wasiojua. Kwa yanga kushinda leo na kuingia raundi ya 2 tumeongeza poit 6 kwenye alama za CAF.

Na hata yanga wakitolewa raundi ya 2 moja kwa moja wanaingia makundi ya kombe la shirikisho, ni heshima kubwa kwa nchi yetu na tunazidi kutetea nafasi zetu 4 vizuri.

Pia nawatakia timu yangu ya Simba kesho izidi kutupa Raha watanzania. Na kwamoto wa simba kesho wasumbiji watatafutana kwa mkapa. Ahaaaaaaa Tanzania Hoyeeee. Yanga, Simba, Azam Hoyeeeeeeee. Tukutane kwa mkapa.
 
Mkuu kwani ulifundishwa uchawi ukiwa na umri gani?
 
Mchaw!
 

Yaani mashabiki wote wa Simba wangekua na akili kama wewe nina uhakika Rage asingejaribu kuwaita mbumbumbu! Tunashukuru sana kwa pongezi na sisi pia Wa kimataifa hatuna budi kuwatakia pia ushindi hiyo kesho.
 
Njoo basi tukutane hapa tupange au umeghairi?
 
Aibu yako mbumbumbu fc
 
Na sisi kesho tunawatakia Ushindi mtani.
Kimataifa tupo pamoja.
Kudos Yanga
Kudos Simba
 
Huwezi kuwa Simba kindakindaki na ukaitakia mema Yanga. Hatutaki shobo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…