Kuna Mtu kule ali ' hack ' ID yangu ila huyu sasa ndiye GENTAMYCINE mwenyewe na nawaomba wote mniamini kwamba Mimi ni mwana Yanga SC mwenzenu hivyo nipeni ushirikino wenu mkubwa ili tuweze kuifunga Simba SC Jumamosi tuzidi kupata raha na kutamba hapa mjini. Na ushirikiano wenu mkubwa wana Yanga SC ninaouomba kutoka Kweni ni kwamba nimesikia Yanga SC imeweka Kambi yake sehemu ya Siri huko Mkoani Morogoro ila Mimi GENTAMYCINE kuna baadhi ya Zawadi kama Maji na Glucose ambazo nimezinunua nataka kuwapelekea Wachezaji wetu wa Yanga SC huko walipo Kambini je kuna Mwana Yanga mwenzetu yoyote labda anaweza akanisaidia kujua Klabu yetu ya Yanga ipo mahala gani na unafikaje huko na mazingira yake yapoje? Ewe mwana Yanga SC mwenzangu ' ushirikiano ' wako wa kunipa malekezo hayo ninayoyataka ndiyo ushindi wetu dhidi ya Simba SC Jumamosi.