Wana Yanga tuishabikie ndugu zetu Simba kwa faida yetu

Wana Yanga tuishabikie ndugu zetu Simba kwa faida yetu

Mimi ni Simba lakini siungi mkono hii kauli wote tushaibikie Simba sababu team ya Tanzania. Hakuna raha ya mpira ni kuwa na watu wanawazomea kidogo wana Yanga wana haki zao kabisa za kushangilia team wanayotaka maana raha yao kuona Simba inafungwa ni kama mimi siwezi kuwaombea Yanga mazuri huo unafiki tu. Team ya kushangili wote in ya Taifa tu sio clubs. Hizi kauli tuungane tushangile team ya Tanzania hazina mshiko na tusi ishi kinafiki mpaka katika michezo. Mimi ni Simba na siwezi kuja kuishangilia Yanga. Tuwaache wana Yanga haki yao kushangilia team yoyote hapo Simba tukishinda wa kuwatukana kwanza hao Yanga hiyo Vita wala hatutawaambia kitu watapanda ndege kuugulia kwao watakaopata shida wana Jangwani. Yanga mimi nawaambia mimi Simba ila msiombe tukashinda mtapata tabu sana mjini tuombeeni njaa tu maneno ya siasa huko eti tuungane...
 
Sisi Yanga kamwe hatutakuja tuwe kitu kimoja na Simba hivyo tumpuuze kwa nguvu zote mtoa mada. Na atayefanikiwa kukutana na mtoa mada amcharaze bakora za kutosha na kumtoa nduki. Ni bora tusishiriki klabu bingwa ila Simba wasiendelee!! Hatuipendi Simba. Vita Club + Yanga nguvu moja,Vita tusaidoeni sana kuwasukumia nje Hawa shwaini
 
Wabongo acheni ushamba bhana,mbona sehem zingine mashabiki wanakuwa pamoja linapokuja swala la maendeleo kwenye soka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza wewe ni mamluki sio shabiki kindakindaki wa Yanga...

Yaani mimi huyo? nitoe vimiguu vyangu nikanunue jezi ya simba niishangilie? Huh, hata kama naumwa siwezi mara kumi nkashabikie misosi Fc kule ndondo cup

Waambie hao Simba hatudanganyiki...

Kila la heri AS VITA CLUB

Sent using Jamii Forums mobile app from my iPhone 5s
 
Salute kwa Simba mpaka walipofika.

Kusema kweli Simba ni club ya kutemela sana hata tz, wamefanya vizuri sana game zao hasa za hapa nyumbani. Ukilinganisha na sisi Yanga ambao tulipangwa kwenye kundi rahisi sana mwaka jana kwenye shirikisho. Japo Simba yupo kama underdog lakin tuwe kitu kimoja na tutoe support ya kweli.

Faida hii hapa. Kama Simba itasonga itakuwa ni mteremko kwa Yanga na Tanzania sababu tutaongeza tumu 1 kwenye michuano hii. Yanga ambao haipewi nafasi ya kuwa bingwa, Simba ikiwa bingwa Yanga ikashika nafasi ya pili moja kwa moja watagombea nafasi ya kushiriki club bingwa Afrika.

Vita club wanatumia jezi ya njano so wanayanga msivae jezi zenu ili kuondokana kama mashabiki wa Vita. Wote tuvae Nyekundu tu.
Asanteni karibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Bilashaka umeandika huu upu upu ukiwa unapumuliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona mnazidi kuweweseka!! Tangu lini shabiki wa Yanga akavaa nyekundu kisa mpinzani wa Simba ana kijani na njano?. Ninawasi wasi uana yanga wako, hatuna shabiki mbovu kama wewe. Hata ingekuwa ni Simba na Mbeya City B sishangilii Simba n'gooooo.

Barafu la moto
Bora niache kushangilia mpira kuliko kuishangilia simba...mambumbumbu fc

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni Simba lakini siungi mkono hii kauli wote tushaibikie Simba sababu team ya Tanzania. Hakuna raha ya mpira ni kuwa na watu wanawazomea kidogo wana Yanga wana haki zao kabisa za kushangilia team wanayotaka maana raha yao kuona Simba inafungwa ni kama mimi siwezi kuwaombea Yanga mazuri huo unafiki tu. Team ya kushangili wote in ya Taifa tu sio clubs. Hizi kauli tuungane tushangile team ya Tanzania hazina mshiko na tusi ishi kinafiki mpaka katika michezo. Mimi ni Simba na siwezi kuja kuishangilia Yanga. Tuwaache wana Yanga haki yao kushangilia team yoyote hapo Simba tukishinda wa kuwatukana kwanza hao Yanga hiyo Vita wala hatutawaambia kitu watapanda ndege kuugulia kwao watakaopata shida wana Jangwani. Yanga mimi nawaambia mimi Simba ila msiombe tukashinda mtapata tabu sana mjini tuombeeni njaa tu maneno ya siasa huko eti tuungane...
Wewe unaakili angalau kidgo kwenye kundi la mambumbumbu umo kwa mkumbo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza wewe ni mamluki sio shabiki kindakindaki wa Yanga...

Yaani mimi huyo? nitoe vimiguu vyangu nikanunue jezi ya simba niishangilie? Huh, hata kama naumwa siwezi mara kumi nkashabikie misosi Fc kule ndondo cup

Waambie hao Simba hatudanganyiki...

Kila la heri AS VITA CLUB

Sent using Jamii Forums mobile app from my iPhone 5s
Hilo anaweza mtafuta kiki Muro tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom