Wanaandamana kupinga kuondolewa kwa wahamiaji haramu Marekani huku wakipeperusha bendera za Mexico, Honduras, na nchi zinginezo

hahahaa,demokrasia bhana inategemea ni nani katenda
 
Wakiinua bendera za Israel sio tatizo ?
 
Hawa wazungu ni wabaguzi tu, hata wao zamani walibaguana sana, na waliishi kwenye makundi yao, kulikuwa na Irish comunity, French, German na zingine kama hizo, baada ya miaka mingi kupita weupe wakajiona ni wamoja.

Hata sasa hao Italian hawawezi kurudishwa kwa rangi yao, watarudisha waafrika, watu wa amerika ya kusini, lakini sio wazungu wenzao.

Sioni na hata hawawagusi hata waandamane na bendera za kichina.
 
Unazijua immigration statuses za wabongo waishio Marekani?
Yes, wengi wao hawana hati sahihi ya kuishi huko na ndiyo maana dada zetu wengi walio huko wanajiuza kwa Nigerians na vijana wetu wakiiba barua za watu kutafuta checks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…