Wanaandamana kupinga kuondolewa kwa wahamiaji haramu Marekani huku wakipeperusha bendera za Mexico, Honduras, na nchi zinginezo

Wanaandamana kupinga kuondolewa kwa wahamiaji haramu Marekani huku wakipeperusha bendera za Mexico, Honduras, na nchi zinginezo

hahahaa,demokrasia bhana inategemea ni nani katenda
 
Huu ni ujinga. Ni upumbavu wa hali ya juu.

Hawa ni waandamanaji wanaopinga sera za Rais wa sasa wa Marekani za kukabiliana na suala na uhamiaji haramu.

Wengi wa hawa waandamanaji ni Walatino.

Hapa ni katika moja ya viunga vya mji wa Atlanta, GA.

Wanaadamana kupigania istihaki [privilege] ya kubaki na kuishi Marekani huku wakipeperusha bendera za nchi walizotoka [au nchi za asili yao].

Upumbavu kama huu ndo unawafanya Wamarekani walio wengi kuunga mkono juhudi za Rais wa Marekani za kukabiliana na uhamiaji haramu.

Utapiganiaje istihaki ya kutaka ubaki na kuishi Marekani huku ukipeperusha bendera ya nchi zingine?

Kama unajivunia sana asili yako ya huko utokako, si urudi/ uende huko ukaishi?

Matendo kama hayo ndo yanasababisha wakose huruma za watu.

Watu wamehatarisha maisha yao ili tu waende kuishi na kufanya kazi Marekani halafu wakifika huko wanaanza kupeperusha mabendera ya mataifa mengine.

Uwendawazimu kabisa huo.

Wahamiaji haramu hawana haki yoyote ile ya kuendelea kubaki Marekani. Warudi tu huko makwao wawe wanalipa kodi huko huku wakipeperusha mabendera yao.

So disrespectful.


View: https://youtu.be/3ARSCXqDpGI?si=mrwqB5UUz2KPDkqc

Wakiinua bendera za Israel sio tatizo ?
 
Hawa wazungu ni wabaguzi tu, hata wao zamani walibaguana sana, na waliishi kwenye makundi yao, kulikuwa na Irish comunity, French, German na zingine kama hizo, baada ya miaka mingi kupita weupe wakajiona ni wamoja.

Hata sasa hao Italian hawawezi kurudishwa kwa rangi yao, watarudisha waafrika, watu wa amerika ya kusini, lakini sio wazungu wenzao.

Sioni na hata hawawagusi hata waandamane na bendera za kichina.
 
Unazijua immigration statuses za wabongo waishio Marekani?
Yes, wengi wao hawana hati sahihi ya kuishi huko na ndiyo maana dada zetu wengi walio huko wanajiuza kwa Nigerians na vijana wetu wakiiba barua za watu kutafuta checks
 
Back
Top Bottom