WanaCCM hebu semeni mnapingana na CHADEMA kwa kitu gani haswa?

Mkwawe

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2016
Posts
3,208
Reaction score
5,682
Katika vitu ambavyo sitaki kuamini ni kwamba CCM wote ni wabaya yaani sitaki kuamini kabisa.

Sasa kama Imani yangu inaniambia Kuna watu wengine wazuri wako CCM Sasa hawa watu wengine wa CCM huwa wanawapinga CHADEMA kwa kitu gani haswa? Kwa sababu hoja nyingi zinazowasilishwa na watu wa CHADEMA zina ushahidi imma wa kutoka ndani ya watu wa serikali (ambao ni CCM wenyewe) au ripoti toka kwa watumishi wa umma na vyombo vya taarifa.

Sasa makada, wakereketwa, wanachama, wadhamini, wapenzi na baadhi ya wafurukutwa wa CCM huwa wanapingana na watu wa CHADEMA ( au upinzani) kwa kitu gani haswa? ina maana watu wema ndani ya CCM hawana nguvu na sauti kabisa katika kuitetea Tanganyika na Tanzania kwa ujumla?

Watu (wote) ndani ya CCM wameridhika na nini hasa?

NB: Watu msiojulikana tunawaomba muache kututeka na kutuua nyie pia ni viunzi (skeletons) watarajiwa
 
Mimi sio CCM ila kuna mambo kibao sikubaliani na Chadema.
 
NB: Watu msiojulikana tunawaomba muache kututeka na kutuua nyie pia ni viunzi (skeletons) watarajiwa
Your browser is not able to play this audio.
 
Mi sio mwanaccm lakini najua wanachokiogopa kutoka chadema ni sera ya ushoga na ukibaraka.
 
Hawataki kuacha kuteka,kunyanyasa na kuua lkn pia ufisadi.
 
Umeleta hoja nzuri sana ndugu mleta mada.
Asante mkuu
Nashindwa kuwaelewa CCM sijui kwanini wanataka kurasimisha kisawe cha neno ushenzi iwe ni CCM
 
Umeleta hoja nzuri sana ndugu mleta mada.
Asante mkuu
Nashindwa kuwaelewa CCM sijui kwanini wanataka kurasimisha kisawe cha neno ushenzi iwe ni CCM
 
Mi sio mwanaccm lakini najua wanachokiogopa kutoka chadema ni sera ya ushoga na ukibaraka.
Bila mihemko ni wapi chadema ilishawahi kujiingiza kwenye harakati za ushoga

Kuhusu ukibaraka ni ushahidi gani unaoonesha chadema wana ukibaraka

Je kati ya CCM na chadema ni nani Kwa macho yaliyo wazi tunaweza kuona kuwa ni kibaraka?
Ukiuza bandari Hadi kiama hiyo ni Kwa ajili ya nani? Kuhamisha wanyama zaidi ya 10000 kwenda uarabuni tena zile spishi adhimu kabisa ni Kwa ajili ya nani?
Kuwatoa wakazi wa ngorongoro na Loliondo Kwa mabavu hiyo ni Kwa ajili ya nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…