Katika vitu ambavyo sitaki kuamini ni kwamba CCM wote ni wabaya yaani sitaki kuamini kabisa.
Sasa kama Imani yangu inaniambia Kuna watu wengine wazuri wako CCM Sasa hawa watu wengine wa CCM huwa wanawapinga CHADEMA kwa kitu gani haswa? Kwa sababu hoja nyingi zinazowasilishwa na watu wa CHADEMA zina ushahidi imma wa kutoka ndani ya watu wa serikali (ambao ni CCM wenyewe) au ripoti toka kwa watumishi wa umma na vyombo vya taarifa.
Sasa makada, wakereketwa, wanachama, wadhamini, wapenzi na baadhi ya wafurukutwa wa CCM huwa wanapingana na watu wa CHADEMA ( au upinzani) kwa kitu gani haswa? ina maana watu wema ndani ya CCM hawana nguvu na sauti kabisa katika kuitetea Tanganyika na Tanzania kwa ujumla?
Watu (wote) ndani ya CCM wameridhika na nini hasa?
NB: Watu msiojulikana tunawaomba muache kututeka na kutuua nyie pia ni viunzi (skeletons) watarajiwa