G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Kusema kweli katika siku ambayo nitachafukwa basi ni siku ambayo Mwamba ataamua tena kurudi ulingoni na kugombea muhula wa tano. Nitachafukwa sana niwe mkweli.
Kama kuna siku nitampa Mwamba heshima yake basi ni ile siku atakayosema kuwa this time inatosha naomba nipishe damu mpya nibakie kuwa mshauri wa mambo mbali mbali ndani ya chama kama mstaafu mashuhuri.
Upo utaratibu wa MACHAWA kuwa wanamchukulia fomu na kwenda kwake kumlazimisha aendelee. Miaka ya nyuma tulimuelewa ila kwa mwaka huu emb ajenge heshima. Ni wakati muafaka kabisa kwa yeye kung'atuka na kweli tutamuheshimu mno, tungeomba hilo litokee.
Kuhusu Zitto tulimuelewa ila kwa awamu hii wapo kweli watu waliopita kwenye tanuru la moto na wanaweza sana kuongoza Chadema na wapo tayari. Wamepikwa wakapikika, Mwamba awape ulingo.
Mimi mpaka sasa sina mgombea ila nasimama na damu mpya na ningeomba wajitokeze wamwage sera tuwapime na tuangalie uzalendo wao ndani ya chama kisha tuvuke na mmoja, ila siyo Mwamba.