Wanaojiita Watanzania waishio nje ya nchi wametangaza kutoa takrima kwa yeyote atakayeripoti habari ya kinachoitwa rushwa kuelekea Mkutano Mkuu wa Chadema Januari 21
Katika Tangazo linalosambazwa limeandikwa;
Ndugu Mjumbe, Mwanachama na mwananchi mpenda haki na Mabadiliko:
Fichua vitendo vya Rushwa kwenye Uchaguzi wa Tarehe 21 kwa kutuma ushahidi wa Rushwa kupitia WhatsApp no. ***************
Kiwango cha rushwa utachopewa utarejeshewa mara mbili kama zawaidi ya Ujasiri wako wa kutetea HAKI
Kampeni yetu ina discourage rushwa kwa namna yoyote. Tunataka viongozi wachaguliwe kwa vigezo, sio rushwa. DIASPORA tumetoa motisha kwa mtu yoyote atakaye tuletea ushahidi wa rushwa usio na shaka, atapewa zawadi. Tutampa mara mbili ya malipo ya hiyo rushwa. #KataaRushwa #SayNoCorruption
Mwisho wa Tangazo
Tangazo hili halina maana yoyote zaidi ya kutaka kuleta uasi, hofu kwa wanachama na kuchochea rushwa ili mgombea wanayemtaka apate kura kwa njia haramu.
Wanachama wa Chadema na wajumbe wa mkutano Mkuu wameshangazwa na jinsi kikundi hicho cha watu wanaojiita Diasspora kinavyotapatapa kujiingiza katika uchaguzi wa Chadema
Kinachozidi kushangaza ni kwamba atakayeripoti kwao rushwa kikundi hicho kitamrudishia mara mbili kitu ambacho pia ni rushwa.
Akizungumza na Taifa leo asubuhi Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alisema kuna kikundi cha watu 30 kinachojiita Diasspora na kinatumika kutukana Chama mitandaoni kuanzia asubuhi hadi jioni.
Haijajulikana lengo hasa la kikundi hiki ni nini, na wana maslahi gani katika mbinu wanazotumia kutaka kuteka Chadema kupitia mlango wa nyuma.
Kikundi hiki mpaka sasa mbali na kutumia mitandao kutukana Chadema na viongozi wake lakini pia wamekuwa wakifadhili na kurubuni baadhi ya wanachama mikoani kutangaza wanamuunga mkono Tundu Lissu na kumkashifu Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.
Mbali na hujuma mbalimbali zinazofanyika mpaka sasa tathmini inaonyesha Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe anatarajiwa kupata ushindi wa kati ya asilimia 60% mpaka 70% ya kura.