McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Watu 38 wakiwemo viongozi, makada na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wameshikiliwa na Polisi mkoani Mara kwa tuhuma za kusababisha vurugu na taharuki katika mji wa Musoma wamepewa dhamana.
Kati ya waliokamatwa yupo Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Pamela Massay. Kundi hilo lilikamatwa Musoma Jumapili Mei 8, 2026 wakati Jeshi la Polisi likichukua hatua za kuzuia kufanyika kwa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yalipangwa kufanyika kitaifa chini ya uratibu wa Bawacha.
Katika tukio hilo, Polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama na wafuasi wa Bawacha waliokuwa wakijaribu kukusanyika kwa ajili ya maadhimisho hayo.
Source: Mwananchi