Mngoreme wa pili
Member
- Feb 22, 2024
- 10
- 10
Na Mwandishi wetu
WAKAZI wa Mchinga mkoani Lindi wamewaonya viongozi wa ACT Wazalendo,iwapo watamchagua Hamidu Bobali kuwa mgombea Ubunge 2025, katika jimbo hilo, kuwa wataelekeza nguvu kwa wagombea wa vyama vingine kuhakikisha Bobali hapati nafasi ya kuwa mwakilishi wao.
Wakizungumza na Mwanakwetu Blogs, wananchi hao kutoka katika kata za Rutamba, Milola, Kiwawa, Mipingo na Kitomanga, wameeleza kuwa Bobali hakuwahi kuwa na Msaada wowote kwa wananchi tokea akiwa Chama cha wananchi CUF.
“Bobali ni mtafuta fursa sisi hapa Lindi tupo pamoja na Chama cha ACT Wazalendo,lakini kwa huyu Bobalik ama atateuliwa na chama basi sisi tutampambania mgombea wa Chama kingine” Alisema Musa Mkambi, Mkazi wa Rutamba.
Saidi Njonjo Mkazi wa Kiwawa,alieleza kuwa Bobali ni mwanasiasa mwenye kutafuta fursa katika vyama vya siasa na sia ajabu akakimbia hata katika chama alichopo sasa.
“Tunamfahamu yule amekuja ACT Wazalendo kutengeneza njia yake lakini hapaswi kuwa sehemu ya waungwana maana alichotufanmmyia wakati akiwa mbunge hatutakisahau na ninaomba Mungu, asipewe nafasi yoyote ya kuja kutuwakilisha sisi wananchi” alisema Msalika mkazi wa Milola
Kwa upande wake Bobali ambaye ni mwenyekiti wa ACT Wazalendo Mkoa alipotafutwa kujibu malalamiko ya wanachama wake,simu zake hazikupokewa