Wanachama CCM Lugata Waandamana Kulaani Viongozi wa Kata Kuzuia msaada wa Mbunge wao Erick Shigongo kujenga Ofisi Mpya

Wanachama CCM Lugata Waandamana Kulaani Viongozi wa Kata Kuzuia msaada wa Mbunge wao Erick Shigongo kujenga Ofisi Mpya

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Lugata wilayani Sengerema mkoa mwanza wameandamana kupiga hatua za viongozi wa chama hicho ngazi ya kata kuzuia ujenzi wa ofisi ya chama hicho ambayo kwa sasa imechakaa na haiwezi kutumika

Hii ni siku ni moja baada ya mbunge wa Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo kufika kata ya Lugata na kuahidi kuijenga ofisi kwa gharama yake mwenyewe.

Wamesema kuwa wao kama wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Lugata wanahaki ya kupata msaada kutoka kwa Mbunge wao ambaye amejitolea kujenga ofisi lakini kuwa na vikwazo kutoka kwa viongozi wa chama hicho ngazi ya kata.

Wameziomba mamlaka husika kuingilia kata Suala hilo ambalo linawanyima haki wanaCCM wa Lugata kupata ofisi safi ya kisasa.


 
Kwahiyo hapo wanaandamana kwenda wap harafu mbona wana weusi wakupauka au hamna mafut
 
Back
Top Bottom