GE2025 Wanachama CCM Masasi wajitokeza kuchukua fomu za ubunge na udiwani

GE2025 Wanachama CCM Masasi wajitokeza kuchukua fomu za ubunge na udiwani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Masasi wamejitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani wa Viti Maalum kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Zoezi hilo limeanza rasmi leo, tarehe 28 Juni 2025, ambapo fomu za ubunge kwa majimbo ya Masasi, Ndanda, na Lulindi zinatolewa na Katibu wa CCM Wilaya ya Masasi, Ndugu Hemed Said Ferej. Kwa upande wa udiwani wa viti maalum, fomu zinatolewa na Katibu wa Umoja wa Wanawake CCM (UWT) Wilaya ya Masasi, Bi. Hilda Selvester Mizengo.

Soma Pia: Uzi maalum wa wanaotia nia kugombea Ubunge Uchaguzi Mkuu 2025

Baadhi ya wanachama waliojitokeza kuchukua fomu ni pamoja na:
• Hadija Utukuru – Jimbo la Lulindi
• Martin Mkanga – Jimbo la Lulindi
• Bwana Hausi – Jimbo la Lulindi
• Abduli Chionda – Jimbo la Masasi Mji
• Dkt. Leonard Akwilapo – Jimbo la Masasi Mji

snapins-ai_3665040837452038715.jpg
snapins-ai_3665040837443807778.jpg
 
Back
Top Bottom