Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Leo nimewaita kuwapa taarifa juu ya hali ya Usalama katika zoezi hilo kama ifuatavyo;-
Kwa ujumla zoezi zima lilikuwa salama wananchi wenye sifa walipata fursa ya kujiandikisha katika Daftari la wapiga kura kupitia vituo vilivyoainishwa katika shehia zao.
WILAYA YA KATI UNGUJA.
Katika Wilaya ya Kati zoezi hili lilifanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 08/03/2025 hadi tarehe 10/03/2025 na hapakuwa na changamoto za kiusalama zilizojitokeza na zoezi lilienda vizuri.
WILAYA YA KUSINI UNGUJA.
Katika Wilaya ya Kusini zoezi lilifanyika kwa siku tatu kuanizia tarehe 11/03/2025 hadi tarehe 13/03/2025. Katika Wilaya hii kwa ujumla wake lilifanyika kwa utulivu na amani ingawa kuna matukio machache yaliyoripotiwa katika vituo vya Polisi kama ifuatavyo:-
- KUZUIA WATU WASIJIANDIKISHE.
- Tarehe 11/03/2025 majira ya saa 4:30 asubuhi huko Jambiani Kibigija wanachama watatu wa ACT WAZALENDO walisimama kwenye njia ya kuingia kwenye kituo cha kujiandikisha na kuwazuia wasijiandikishe kwa madai kuwa watu hao wana asili ya Tanzania Bara huko wakijua kuwa hawana mamlaka ya kufanya hivyo watu hao ni:-
- RAMADHAN HASSAN RAJABU, 58 yrs, Mshirazi, Mvuvi wa Jambiani Mzuri.
- MOHAMED PANDU VUAI, 43 yrs, Mshirazi, Mvuvi wa Jambiani Mzuri.
- AMEIR KISHAJI AMEIR, 60 yrs, Mshirazi, Fundi Mwasi, Mkazi wa Jambiani Mzuri.
- KUWANYANG’ANYA WANANCHI VITAMBULISHO.
- Mnamo tarehe 11/03/2025 majira ya saa 03:30 asubuhi huko Nganani Makunduchi katika eneo la uandikishaji wapiga kura, wanachama wa ACT WAZALENDO waliwakamata watu wawili na kuwanyang’anya vitambulisho vya Mzanzibar watu hao wanatafutwa na Jeshi la Polisi ili wakahojiwe juu ya kitendo hicho ambacho lengo lake ni kuvuruga zoezi la uandikishaji; walionyang’anya vitambulisho ni EMMANUEL KINYAJA SAPILI, 42 yrs, Mkazi wa Nganani Makunduchi na Mkewe ELIZABETH KULWA, 21 yrs
- KUZUIA WATU WASIJIANDIKISHE.
- Mnamo Tarehe 11/03/2025 majira ya saa 3:30 asubuhi huko Muyuni ’A’, mwanachama mmoja wa ACT WAZALENDO aitwaye KHAMIS HAJI JUMA, 56 yrs, Mshirazi WA Muyuni ’A’ bila mamlaka aliwazuia wafanyakazi wake kwenda kujiandikisha kitendo ambacho ni kuwanyima haki yao ya kikatiba: Wafanyakazi hao ni;- EMASON ARIN YINGA, 25 yrs, Muha, Mkazi wa Muyuni na mwenzake ISSAYA s/o WILBERT ZINJIBAR, 37 yrs, Muha, Mkazi wa Muyuni ’A’. Mtuhumiwa amekamatwa na kuhojiwa.
- KUFANYA FUJO KWENYE KITUO CHA KUANDIKISHA WAPIGA KURA.
- Mnamo tarehe 11/03/2025 najira ya saa 05:30 asubuhi huko kituo cha kuandikishia TASAN mwanachama ALLI s/o ABDALLA MKWENDE alifanya vurugu kwa kutoa lugha za vitisho na kuwapiga picha watendaji wa kituo hicho kitendo ambacho kililenga kuvuruga zoezi la uandikishaji. Mtuhumiwa alikamatwa na kuhojiwa.
Imetolewa na:-
Daniel E. Shillah-SACP,
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Kusini Unguja.
Daniel E. Shillah-SACP,
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Kusini Unguja.