Wanachama wa CCM Itumbi waipokea kwa shangwe kauli ya Waziri Mkuu Majaliwa. Sasa tume ya madini ifute PL/ 6973/2011 haraka

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Tume ya madini, kama mmemsikia majibu ya waziri Mkuu aliyotoa Bungeni leo Aprili 18, 2024, basi msiwe na kigugumizi kuhusu kuifuta PL/6973/2011.

Sababu za kuomba ifutwe na kukubaliana na kauli ya waziri Mkuu hizi hapa:

1. Ilisha kwisha muda wake.

2. Ishapewa au kutengewa wachimbaji wadogo.

3. IPO kwenye makazi ya watu na taasisi za serikali.

4. Wanao chimba kwenye maeneo yaliyo ndani ya hiyo PL hawalipi mirahaba Kwa kigezo kuwa hawana leseni.

5. Hiyo PL hajawahi kulipiwa na Ina madeni na malimbikizo ya mamilioni .

6. Walioomba maeneo ambao ni wachimbaji wadogo, wamezuiliwa kupewa na kulipia leseni zao, sababu kubwa ikiwa ni kusubiria PL ifutwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…