Wanachama wa CCM mnaposhangilia ushindi mkumbuke kuwa kuna kipindi kigumu cha maisha kinakuja mbele yetu

Wanachama wa CCM mnaposhangilia ushindi mkumbuke kuwa kuna kipindi kigumu cha maisha kinakuja mbele yetu

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari,

Kuna watu wanajua ila wanajisahaulisha kuwa nchi za Magharibi ndizo zinazotusogeza mbele au kutusapoti kwenye sekta ya Afya na Elimu kwa kiasi kikubwa.

Hii iko wazi miaka na miaka.

Watu wa Magharibi hakuna kitu wanajali kama Demokrasia ambayo imeminywa kwa miaka 5 yote ya Magufuli. Akaachia miezi 2 ya campaign na jana umefanyika uchaguzi wa kiini macho.

CCM wameshinda kwa kishindo. Hiki kishindo haramu kitawafikia sponsors huko Ng'ambo na ndipo watajitoa kusapoti mambo muhimu. Hapo tutaanza kuuziwa huduma zote za afya kwa bei kamili. Hapo ndipo elimu yetu itatikisika.

Uchumi utayumba, hapa mwananchi wa kawaida, mtumishi wa umma wa kawaida, mfanyabiashara mdogo na wa kati, mkulima n.k lazima ataisoma.

Tushangilie na kupongezana ila tutambue kuwa kikija kipindi kigumu hao viongozi wakuu hawatapata taabu.
 
Wewe ndio upate wasiwasi huo.. Nchi inathaminika sanaaaaaaa
kwasababu ya JPM..
Unataka waweje.. wakae wawe wavivu kama wachache nyie...
wengi mulitaka muanze kuiba tu pesa za umma.. hakuna
lingine kabisaaaaa...

nendeni mkachukue vya 20K muanze biashara... asiyefanya kazi na.....
 
Mkuu usitishe wananchi, maelezo km haya pia muliyatoa Znz katka ule uchaguzi wa marudio.
 
Tumewazoea na Matamko na tabiri zenu kila siku zisizotimia.

People's power lazima iheshimiwe. Uchaguzi umefanyika salama kabisa,Pia kula zinahesabiwa mbele ya mawakala wenu,
Kwahiyo CHADEMA mlitegemea mtaishinda katika Uchaguzi huu??

I think you are too disappointed, Sababu mlikuwa na matarajio makubwa bila strategies zozote.
 
China wameshajipanga kuwa upande wa Tz. Sikilizeni, if you can't change the situation, adapt. Anzeni sasa kusifia, shindaneni kusifia na MATAGA, anzeni kugombania mkate wao.
 
Nyie ni Wapumbavu sana, Dunia nzima inaelewa na inathamini mchango na uongozi wa Magufuli. Hicho kipindi kigumu unachosemea umekaririshwa tu, miaka mitano iliyopita tuli survive vipi?, Au ulikuwa nje ya nchi?

Umiza kichwa maisha ndo yalivyo, hakuna Rais atakayekuja kuwaletea mkate mezani. Upinzani wa kupinga kila kitu bora utokomee kuzimu tu. Mmedanganywa na wanasiasa eti tunataka maendeleo ya watu sio vitu na nyie mkazungusha viuno.

Ila nawashukuru sana wananchi sio wajinga wamewanyoosha kwenye box la kura na huyo mnyoa panki wenu. Narudia wananchi sio wajinga wanaona aliyoyafanya Magu heshima ya mwananchi wa kawaida umerudi kipindi hiki cha Magu. Watu wamesogezewa huduma muhimu nyie mnabeza eti maendeleo ya vitu, nani awape kura?
 
Maisha ya wanaCCM yatakuwa neema tupu. Watakula kuku kwa mrija
 
Maisha magumu ni ya kwenu watoa povu maana mna miaka 5 tena mbele ya kubwabwaja mapovu kwenye mitandao
 
Back
Top Bottom