DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) zaidi ya 50 kutoka kata ya Minepa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro wameandamana katika Ofisi ya Mkoa ya Chama hicho, kwa madai ya kutoridhia uamzi wa jina la mgombea wa nafasi ya udiwani aliyeshinda kwenye kura za maoni kutorudishwa, wakishinikiza kurudisha kadi za uanachama endapo malalamiko hayototekelezwa.
Hussein Ndalama, Hamis Mstapha na Aloyce Makindaga ni miongoni Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Minepa ambao wamefika Ofisi ya Chama hicho Mkoa wa Morogoro, wameamua kufika kwenye ofisi hiyo ili kupata majawabu ya maswali yao, ikiwemo mgombea aliyeshinda katika kura za maoni kwa 174 kutopewa barua ya utamabulisho badala yake amepewa mshindi wa nafasi ya pili aliyepata kura 168.
Malugu Manosu ni mshindi wa kuwania nafasi ya udiwani kwa Kata ya Minepa katika mchakato wa kura za maoni, anaeleza hatua aliyochukua baada ya kupata taarifa ya kuwa jina lake limeenguliwa.
Akizungumza kwa njia ya simu Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Nuru Ngereja kutolea ufafanuzi sakata hilo, amekiri kutambua suala hilo, akihimiza wanachama hao kuwa watulivu kwa kuwa jambo hilo linashughulikiwa na makao makuu.