Sekretarieti ya Klabu ya Simba imewafungia kujihusisha na masuala ya klabu Wanachama Mohamed Khamisi Mohamed maarufu Dr. Mohammed na Agnes M. Daniel maarufu Aggy Simba mpaka pale kamati ya maadili itakapoamua vinginevyo.
Sekretarieti imepokea malalamiko mengi ya kimaadili dhidi ya Wanafamilia hao wa klabu ya Simba ikiwemo kuitisha mikutano kinyume na taratibu na kuchochea migogoro ndani ya Klabu.
Sekretarieti itawafikisha Wanachama hao mbele ya Kamati ya maadili hivi karibuni.
Uamuzi huo umefikiwa kwa Mamlaka ya Sekretarieti iliyonayo chini ya Ibara ya 31(4)(g) ya katiba ya Simba ya klabu ya 2018 (kama ilivyofanyiwa mareke- bisho 2024), katika kuhakikisha Mahusiano ndani ya Klabu, Wanachama, na Mashabiki hayaathiriwi.
Sekretarieti inawakumbusha wanachama na mashabiki kuheshimu Katiba, Kanuni, na Miongozo iliyopo ndani ya Klabu.
Imetolewa na Sekretarieti, Simba Sports Club Juni 15, 2024
View attachment 3018081