Wanachama wa Simba 'Aggy Simba' na Dkt. Mohammed wafungiwa kujihusisha na klabu kwa muda

Kazi kweli kweli kwenye mambo ambao yanagusa ugali wa mtu basi sheria inafanya kazi ila sheria za kuwaondoa madakani kwa kuboronga hapo sheria hazionekani.Tusishangae mashabiki tukapewa kesi za kuwa sisi ndiyo tumesajili pia wachezaji wabovu.
Comrade, hii hoja ulitakiwa kuitoa siku ile ya mkutano wenu mkuu. Ila ndiyo hivyo tena; lile pilau la Mangungu na ule ujio wa Manzoki kama mshereheshaji mkuu wa mkutano! Ukawatoa kabisa kwenye reli.
 
Ngoja inyeshe.
 
Kuna taratibu za kuitisha mkutano wa dharula, swali je wanachama Hawa waliufata Kama hawakufata walikuwa na malengo gani? Huenda walikuwa wanatumiwa na watu kwa malengo yao Ila ngoja tusikilize na upande wa pili.
 
Sijawahi kumkubali Mangungu wala Salim ila huyo Mohamed naye anajikutaga kama msemaji wa timu, alitakiwa afungiwe siku nyingi sana au apewe onyo kuiongelea klabu kama vile ni msemaji wake.

Huyo Aggy naye alitakiwa awe amepewa onyo muda mrefu uliopita kwa tabia ya kuiba kila content ya Simba Instagram na kuiweka kwake bila kutoa credit.

Nasimama na kauli yangu ya muda mrefu kuwa itachukua muda mrefu sana Simba kuja kutulia tena na nina sababu zangu za msingi kusema hivyo. Hawa mashabiki wenye mvuto wote ni virusi tu, wananunulika na upande wowote kuyumbisha muelekeo sahihi wa timu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…