Wanachama wengi wa JamiiForums ni mashabiki wa TBC1

Wanachama wengi wa JamiiForums ni mashabiki wa TBC1

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2010
Posts
4,845
Reaction score
4,776
Nianze kwa kulipongeza shirika letu la utangazaji Tanzania kwa maboresho makubwa katika vipindi, teknolojia na ubunifu hususani katika awamu hii ya 5. Tumeshuhudia maana hasa ya shirika la utangazaji la UMMA.

Katika jukwaa hili wapo wengi ambao hujinadi kuwa hawaitazami kabisa TBC1 lakini baada ya utafiti nimegundua kuwa wanachama kama G Sam na genge lake ni mashabiki wakubwa wa TBC1 na wanafuatilia vipindi karibia vyote ndomaana katika ukosoaji utasikia kipindi fulani kinashida hii kipindi kingine kina shida ile mara kwenye ARDHIO mtangazaji fulani alifanya hiki nk

Hilo linaniambia kuwa TBC1 ni baba lao. Mimi ni mpenzi sana wa vipindi vinavyoonesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ambavyo Zitto hutamani ardhi ipasuke afiche aibu anapofuatilia TBC1 na kuona Rais Magufuli anavyoibadili nchi hii katika miundombinu kila kona mpaka huko Kigoma.

Najua mitambo mipya karibu itazinduliwa na TBC itakuwa zaidi hata ya TV za mabeberu katika kila sekta.
 
Wanasema hata makaburu walitekeleza miradi mikubwa Sana na bado walipingwa na kufukuzwa
 
binafsi hata redio yao huwa nasikiliza, kwasababu kuna uwezekano mkubwa wa kujifunza vitu vipya ukifuatilia vipindi vyao. Na JUNGU KUU ya saa 3 na robo hivi ni my favourite
 
binafsi hata redio yao huwa nasikiliza, kwasababu kuna uwezekano mkubwa wa kujifunza vitu vipya ukifuatilia vipindi vyao. Na JUNGU KUU ya saa 3 na robo hivi ni my favourite
Ahsante, Chadema nao wanasikiliza kwa sauti ya chini wakija huku wanabisha
 
Yaani kabisa tuwe busy kuangalia TBCCM! Halafu kila siku mnajisifia kuzindua hiyo inayoitwa "mitambo mipya"! Na ile mliyobambikwa na Wachina kupitia Kampuni yao ya Startimes mtamuuzia nani?
Kumbe wewe ni mfuatiliaji mzuri wa TBC mpaka unajua mikataba, usikose kipindi cha ARDHIO leo kuanzia sa1 kamili jioni
 
Kumbe wewe ni mfuatiliaji mzuri wa TBC mpaka unajua mikataba, usikose kipindi cha ARDHIO leo kuanzia sa1 kamili jioni

Siku mtakapo achana na mapambio na hivyo kusimamia maadili ya kazi yenu, huku mkiifanya hiyo TBC kuwa mali ya Watanzania wote! hakika nitawaangalia muda mwingi tu.

Ila kwa sasa mtanisamehe. Maana hamna kabisa tofauti na Channel ten. Bora hata Utv na ITV ila siyo TBC.
 
Ulijuaje kama si kwa kuangalia? Hongera kwa uzalendo, hata leo najua uliangalia.
 
Back
Top Bottom