Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 23,566
- 24,891
Katika mkutano wao mkuu, kilitokea kioja ambapo watu wazima walitokwa na aibu na kuamua kujidhalilisha hadharani kwa kuamua kupiga magoti na kumlilia YM ili kumuomba agombee tena uenyekiti. Bila shaka wamepiga mahesabu, mahela yote haya wameshindwa kulipa kisasi cha 5-0, badala yake wameendelea kupigwa tu 3-1, sasa je bila hela si zitakuwa 7-0 ??? Pia kuna maswali wanajiuliza, wamesajili mastaa kibao kutoka Simba kwa mikataba ya kuwalipa mishahara mikubwa mikubwa, sasa nani atakuwa anawalipa mishahara wachezaji? Watu wazima wenye watoto nyumbani wakaamua kumpigia magoti mtoto mdogo, lakini jamaa amegoma! Kazi kwenu Jangwani