Wanachokifanya Marekani na NATO kwa ujumla dhidi ya Urusi ni sawa na kumbana paka kwenye kona; atakachokufanyia utakisimulia masha yako yote

Warusi wa Kisukuru na Nangulukulu mbona hamuelewiki? Jukwaani humu mnahubiri vikwazo vya Magharibi na US havina athari yoyote kwa uchumi wa Urusi, gafla vimeanza kukaba koo?.
Putin ana kichwa kibovu, ila nakuhakikishia hawezi igusa Marekani au Uingereza. Hizo nuclear wapinzani wake wanazo mpaka za kuonja, siku akijichanganya kwa NATO ndio utakuwa mwanzo wa Urusi kuungana na club ya Libya, Afghanistan na Syria.
 
Dunia sio sehemu salama.
Itafikia wakati binadamu mwenyewe ndiye atakaye i destroy hii dunia.
Maana akilizi ikizidi mtu anashika mavi
Binadamu ndio wameharibu hii dunia, isingekuwa na watu ingekuwa ni eneo zuri zaidi.
 

Asubuhi Hii personal banker wa Putin yamemkumba
 
Wanachokifanya Marekani, NATO na mataifa ya magharibi kwa ujumla dhidi ya URUSI ni kuifunga mikono na miguu URUSI wakati ikipigana na UKRAINE, ili kumbieni warudi nyumbani kabla hawajachelewa!! Mark my words!!
habari za kusadikika, hakuna wa kumtishia mwenzie nuclear kwan wote wanazo,
 

Na wote tuseme amen
 
Yaani mimi kiongozi wa nchi akishakuwa dikteta , mwenye tamaa ya madaraka akibadili katiba ili aongoze milele, na kuwaongoza wananchi wake kwa mkono wa chuma siwezi kumkubali kamwe! Na hicho ndicho kinatofautisha hao 'mabeberu ' na hao madikteta wanaoshabikiwa humu.

Watu wamejazana humu wanamshabikia Putin, Kim Jong Un, Xi Ji Ping na madikkteta wengine wakati jiwe aliwaonjesha moto kidogo tu ukawa mtafutano. Mswahili ni mtu wa ajabu sana!

Ubaya wa hao madikteta wanawaziba midomo raia wao, kwahiyo ukiwa buza au kyaka huwezi jua ni namna gani wanataabika. Leo hii tunawashangilia hatujui raia wao wanawasapoti ama wanawachukia kiasi gani, hakuna uhuru wa mawazo/maoni. Ndio maana hata umasikini uliowang'ang'ania hao wananchi wao hatuujui kwa sababu hakuna nafasi ya kuupata vema. Wengi wetu huma tunaamini hizo nchi zote ni tajiri sana. Niliwahi sikia kuwa North Korea hata umeme kukata ni kawaida sana, ila humu utasikia kiduku kiduku balaa!

Unapomshabikia dikteta imagine kwanza hata hali za raia wake chini ya msoto katika karne hii ya 21.

Wabongo tunapenda kuwashabikia madikteta wakiwa kwingine, ila udikteta ukiingia kwetu ndo tunaanza kuchambua takwimu za demokrasia. Kwa sasa tuna amani umesahau kabisa.

Ukiwachukia wa magharibi angalau kuwa neutral tu basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hi I nyie hizi habari mnazipatia wapi? Leo kuanzia cnn, times, BBC , aljazeera.. wameamua kusema ukweli Russia wanafanya unyama kyv imekaribia kuangamia hesabu siku 7 hivi Rudi humu utatuambi
 
Hi I nyie hizi habari mnazipatia wapi? Leo kuanzia cnn, times, BBC , aljazeera.. wameamua kusema ukweli Russia wanafanya unyama kyv imekaribia kuangamia hesabu siku 7 hivi Rudi humu utatuambi
Leo 16 mkuu.,
 
Ni saw na kuachana je unamwagia tindikali.??
 
Hivi karibuni china ataongoza dunia kiuchumi zaidi ya U.S.A,hili la vikwazo limemgarimu sana.
 
Licha ya ukraine kupewa air defense system,anti-tanker na u.s.a,lakini mrusi anapenya tu,juzi waliomba vita isimame kwa muda ili wabuni mbinu mpya wakaambiwa hakuna huo muda hao wananchi waliobaki washike silaha..
 
Hapo ndo tunasema ukimbana paka kwenye kona ni hatari sana! Putin anaweza kufanya chochote huku akijua kuwa vita ya nyuklia haina mshindi! Ni maangamizi kwa wote! Busara ni kumwondolea vikwazo na kumtoa kafara Ukraine!
 
Hapo umenena!! Ukraine ametumika kama chambo tu! Mabeberu ni kwanza maslahi!
 
Haya waulize Walibya! Walidanganywa kuwa Gaddafi ni dikteta, anajilimbikizia Mali, mkimwondoa mtapata raha sana! Wakarubunika, wakamwasi Gaddafi na wakamwua!! Leo Walibya wanaishi maisha ya umaskini na marekani yuko pembeni akiwacheka! Wakti wa Gadafi maji na umeme vilikuwa bure, posho kubwa kwa kila asiye na ajira, ukioa unapata posho maalumu, pia kila ulipata mtoto unapata posho!! Leo vyote vimeota mbawa! Wanatamani Gaddafi angefufuka lakini haiwezekani! Hao ndio mabeberu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…