Wanachopaswa kufanya CHADEMA baada ya Tamko la Polisi

Wanachopaswa kufanya CHADEMA baada ya Tamko la Polisi

Toka asubuhi nimeona taarifa za hamasa za kumpokea Tundu Lissu. Ni katika kuhamasisha mipango ya ndani ya Chadema kumtengenezea ukubwa Tundu Lissu, lakini nasikitika kusema Chadema wamefeli kwanzia planning, na execution ya Jambo la Lissu.

Nitaelezea siku nyingine hapo kwenye planning ila kwa haraka haraka, tayari walishajua kuna msiba wa kiongozi (former President) Mh Mkapa ni tukio zito katika level ya Taifa.

Alikuwa na nyadhifa mbalimbali, Rais, Mwenyekiti wa CCM na pia Amekuwa Amiri Jeshi mkuu. Attention ya taifa ni huko, Lissu anakuja kama mtu ambae anajinadi anataka kuongoza nchi, ile ni nafasi kubwa inabidi ajiweke (act as the one), kama mtu ambae atakuwa baba, mfariji na kiongozi wa wote.

Angekuja bila hyping au mbwembwe aelekee uwanja wa uhuru au nyumbani kwa Hayati Mkapa, ila kwa sababu CHADEMA hawana mipango na wao sio wanasiasa ni wanaharakati wanatafuta mob attention. Hakuna nchi inayoweza kuruhusu hilo. Msiba wa Rais (former), unatambulika kikatiba.

Ninachojua CHADEMA hawashauriki na wanapenda kushupaza shingo ila warudi wajiangalie upya.
TL pia anamoyo kama binadamu mwingine. Alipopigwa lisasi 16 hata pole hakupewa wakati hawa ndiyo wafariji wenyewe. Sasa aende uhuru moja kwa moja kwa lipi!!
 
Kugoma kwenda taifa kwa sababu hatafufuka hiyo ndiyo uanaharakati ndani ya Chadema. Ila pamoja na kwamba kanusurika kuuawa anarudi kama mtu ambae anataka kuwa Rais “siasa” ni kwenda kutoa pole.. unless uniambie Lissu hayupo serious na nafasi ya urais.
Kwani umeambiwa ndege itatua msibani? Lissu atatua kwanza iwe kimya kimya au kwa mbwembwe haijalishi, halafu baadaye atakwenda msibani kama wengine. Tena hapo msibani hapatatosha wasipokuwa makini wajue Lissu sasa ni zaidi ya mwanasiasa.
 
Umetoa ushauri mzuri sana.... lissu anahitaji mapokezi sema huu msiba ni mkubwa sana..
Msiba mkubwa kwa nani? Sisi malofa na wapbavu bila ya kusahau Wapemba wahanga wa tukio la 27 Jan 201 hautuhusu. In fact siku ya saba tunachinja na kusheherekea Eid jwa hiyo sherehe juu ya sherehe.

By the way, kwa nini uwe ni msiba wakati mtu kaishi maisha beyond everyones expectations, ka achieve more than one would hope for, a life well and long lived.
Why mourn instead of celebrate his life! Hii tabia ka kuomboleza ni ukosefu wa shukurani kwa Muumba. Hata kama una smart phone chako kikifa baada ya miaka 5 na ushakitumia sana kwa online shopping hutakiwi usikitike!
 
Angekuja bila hyping au mbwembwe aelekee uwanja wa uhuru au nyumbani kwa Hayati Mkapa, ila kwa sababu CHADEMA hawana mipango na wao sio wanasiasa ni wanaharakati wanatafuta mob attention. Hakuna nchi inayoweza kuruhusu hilo. Msiba wa Rais (former), unatambulika kikatiba.
Hivi kwa akili yako unaona kabisa policcm watamruhusu aende uwanjani au nyumbani kwa Mkapa? Thubutu!! Kumbuka wakati wa kampeni Lowassa alizuiliwa kwenda kumzika Kisumo, sasa huu ujio wa Lissu wakiruhusu aende uwanjani watu watahamishia masikio kwake! Hicho kitu serikali yangu haitaruhusu!
 
Kugoma kwenda taifa kwa sababu hatafufuka hiyo ndiyo uanaharakati ndani ya Chadema. Ila pamoja na kwamba kanusurika kuuawa anarudi kama mtu ambae anataka kuwa Rais “siasa” ni kwenda kutoa pole.. unless uniambie Lissu hayupo serious na nafasi ya urais.
Wewe umekwenda na watanzania wote kutoa hiyo pole!
 
Back
Top Bottom