Wanachuo; katika wakati huu ambao mmeshapokea/mnasubiri kupokea fedha za kujikimu (BOOM), jaribu kuwa na mpango mzuri wa matumizi, kuepuka kuingia katika hali ngumu ya kifedha baada ya muda mfupi na hata kutumbukia kwenye madeni. Nilishuhudia mwanafunzi wa chuo (binti) akikamatwa supermarket kwa kuiba, katika wiki hili, katika vyuo vingine kumekuwa na taarifa za wizi (hata kwa kutumia silaha - mapanga,visu) kati ya wanachuo wenyew; haya yote yanatokea baada ya BOOM kukata na maisha kuanza kuwa magumu. Mabinti wamekuwa wakienda kumbi za strarehe na kujaribu kuweka mitego.
Tukumbuke ule usemi "PESA INAONGEA", usemi huu ni dhahiri ndugu zangu; utakuta unapo-pokea fedha tu mipango yote mizuri utashangaa inatoweka na mawazo mapya yanakuja, PESA inasema na wewe, "twende tukanunue ngou", "twende club", "twende tukanywe na washikaji" na mengineyo mengi. Jitahidi kuheshimu na kusimamia mpango wako wa Matumizi. Usiangalie wengine wanaishi vipi?, mpango wako wa matumizi, ndio maisha yako.
Usiishi kwa imani ambayo baadae haitatenda kazi, kwamba zitapatikana nyingine. Kutoka wapi.......????, hapo ndipo wengine wanapojikuta wameangukia kwenye vitendo vibaya kama wizi, umalaya, na mengineyo. Epuka kabisa kufanya mpango wa matumizi kwa pesa ya kutarajia....FROM SOMEWHERE...????. Hakikisha una FOCUS kwa hicho ulichonacho.
Vile vile unaweza kufikiri jinsi ya kuongeza pesa uliyonayo, hata hapo chuoni unaweza kufanya jambo la kuongeza kipato chako (THINK..). Itakusaidia kuwa na uhakika wa kipato chako, badala ya kuwa zinatoka tu.
Jitahidi kutokutembea na pesa taslimu (mfukoni/begi) amabzo hujapanga kwa siku hiyo zitakuwa na matumizi gani ni rahisi kushawishika kufanya matumizi ambayo hujapanga, kama siku kuna utamaduni wa vitu kutembezwa mitaani, hivyo unapokuwa na pesa ambazo hazina matumizi ni rahisi kushawishika kununua.
Naamini wengine wataweza kuongeza yale ambayo yatatusaidia katika kuwa na akiba ya fedha za kujikimu chuoni katika muda husika, kutokana na uzoefu......KARIBU......!!!