Wanachuo MUHAS wanazimiwa AC na WiFi Ila wakiwemo wasudan zinawashwa

Wanachuo MUHAS wanazimiwa AC na WiFi Ila wakiwemo wasudan zinawashwa

Bongo bahati mbaya aisee😁😁 wabane meno tuu wamalize muda wao watembee, ndio maana Tanzania inasifa nyingi za ukarimu nje ya nchi ambazo sisi wenye nchi tukizisikia tunajibana tusicheke tuu 😁😁
 
Hivi tabia za roho mbaya huwa zinaanza na malezi ya nyumbani. Wazazi wanalea watoto kwa mtindo wa kutowapa treatment nzuri au care ila anapokuja mgeni watoto wanashuhudia mgeni akipewa care nzuri. Mifano hai ipo,

Mgeni akija atanunuliwa soda kitu ambacho wazazi huwa hawana kawaida ya kufanya kwa watoto wao.

Mgeni atachinjiwa kuku au kuandaliwa chakula kizuri sana ambacho watoto inaweza pita mwaka hawajakiona.

Mgeni akija sebuleni patafanyiwa usafi wa hali ya juu kwaajiri ya kumpokea ila watoto wamezoea kuona sebule ikiwa haipo nadhifu.

Mgeni atakuja king'amuzi kitalipiwa kifurushi kikubwa wakati kawaida watoto huwa wanatazama local channels tu hapo ndani.

Mgeni atatandikiwa shuka zuri na safi sana tena jipya siajabu watoto wanalalia shuka za zamani. Na ikibidi hata godoro mpya inaweza nunuliwa.

Watoto wakiona hivi vitu hata kwenye akili zao wanaamini kuwa wao sio watu muhimu hadi kwenye jamii. Wakitoka na kuingia uraiani wanaendeleza ule utamaduni wa unyonge na kutostahiki kupewa vitu vya msingi au vizuri. Matokeo yake tunakuwa na kizazi cha watu makabwela wanaokubaliana na maisha ya chini na yasiyo na hadhi.

Ndio maana watanzania kudai haki ni wavivu sana. Barabara mbovu, umeme unakatwa hovyo, maji ya mgao, hospital huduma za utata, na kadhalika ila wanashinda kuchukua hatua sababu wamefunzwa tokea majumbani kuridhika na kuvumilia kupewa wasichostahiki au kupokea wasichoridhika nacho.

Haya malezi tuachane nayo kizazi chetu kisilee watoto kikabwela.

Mzazi mara moja moja watoe out watoto wako kwenye hotel nzuri. Wananulie zawadi na kuwaambia ni matokeo ya tabia nzuri na adabu zao nzuri.

Kwenye friji mazaga kama juice za kutengeneza nyumbani zisikose. Mkeo ajifunze kutengeneza keki, cookies, bites, awe anawatengenezea watoto. Na mara moja moja unanunua crate au katoni ya soda unaweka kwenye friji madogo wasikae kinyonge wakiona watu wanakunywa huko nje.

Watoto hakikisha wanalalia shuka safi, magodoro yabadulishwe kwa wakati. Na mavazi wawe nadhifu.
 
Maneno matupu bila ushahidi watu mnaandika paragraphs.
Lakini Hizi tabia huanzia majumbani Mgeni akija mnachinja kuku.
 
Hii kali sana kweli ngozi nyeusi ni nyeusi tu..

Rafiki yangu aliepo MUHAS, katika story za hapa na pale akawa ananielezea kuwa licha ya JOTO la Dar hili lote madarasa wanayotumia kusomea na yenye WiFi huwa yanawashwa AC tu ikiwa hawa wanafunzi wageni wa SUDAN wakiwa wanafundishwa .. (ikumbukwe madarasa/lecture rooms wanashare wote).. wakitoka tu ama vipindi vyao vikiisha walinzi wanakuja kuzima AC ..zinazimwa ukijaribu kuuliza unaambiwa nyie sio watu maalum tumepewa maelezo AC ni kwa ajili ya wanafunzi wa Sudan..

Ikumbukwe wanafunzi hawa wa Sudan wapo MUHAS kusoma sababu ya hali ya kiusalama nchi kwao kuwa sio nzuri wamekuja huku ili kuendeleza masomo yao ambayo walikuwa wanasoma..

Namnukuu.
.
"Kama sisi watu weusi tunafanyiana hivi, kuna haja gani ya hawa waSUDAN wawepo? Bora wasiwepo ili tuendelee kupambana na joto" sisi ngozi nyeusi tuna shida gani hasa tukiona ngozi nyeupe? Upo radhi umkandamize mwenzako kisa sio mweupe?
"
Mwisho wa kunukuu..

Waungwana hii ni sawa?..
Ngozi nyeusi haiathiriwi na joto kali.
 
Special occasion Ni muda wa wanafunzi wa Sudan wakiwa wanasoma tu, wakiingia wanafunzi wa MUHAS wanazimiwa..? Mbona wakati hawajafika waSUDAN AC Zilikuwa zinatumika.. muda wote. Kwani waSUDAN wamebadili nini?

Msiwafanyie vijana hivyo hata wao wanalipa ADA .. Joto la DAR hili lote bado unawafanyia watoto hivyo wewe ungekubali? Ufanyiwe hivyo ilihali AC ziliwekwa sababu ya matumizi hayo.
Wakitoka hapo hao wanafunzi hawana uelewa wowote, ndo wanakuja field hospital kuua wagonjwa, Lol
 
Bongo bahati mbaya aisee[emoji16][emoji16] wabane meno tuu wamalize muda wao watembee, ndio maana Tanzania inasifa nyingi za ukarimu nje ya nchi ambazo sisi wenye nchi tukizisikia tunajibana tusicheke tuu [emoji16][emoji16]
Kabisaaa yaan [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Utamu wa taifa hili wanaujua wageni, kuliko wenyejii.
 
Back
Top Bottom