Hivi tabia za roho mbaya huwa zinaanza na malezi ya nyumbani. Wazazi wanalea watoto kwa mtindo wa kutowapa treatment nzuri au care ila anapokuja mgeni watoto wanashuhudia mgeni akipewa care nzuri. Mifano hai ipo,
Mgeni akija atanunuliwa soda kitu ambacho wazazi huwa hawana kawaida ya kufanya kwa watoto wao.
Mgeni atachinjiwa kuku au kuandaliwa chakula kizuri sana ambacho watoto inaweza pita mwaka hawajakiona.
Mgeni akija sebuleni patafanyiwa usafi wa hali ya juu kwaajiri ya kumpokea ila watoto wamezoea kuona sebule ikiwa haipo nadhifu.
Mgeni atakuja king'amuzi kitalipiwa kifurushi kikubwa wakati kawaida watoto huwa wanatazama local channels tu hapo ndani.
Mgeni atatandikiwa shuka zuri na safi sana tena jipya siajabu watoto wanalalia shuka za zamani. Na ikibidi hata godoro mpya inaweza nunuliwa.
Watoto wakiona hivi vitu hata kwenye akili zao wanaamini kuwa wao sio watu muhimu hadi kwenye jamii. Wakitoka na kuingia uraiani wanaendeleza ule utamaduni wa unyonge na kutostahiki kupewa vitu vya msingi au vizuri. Matokeo yake tunakuwa na kizazi cha watu makabwela wanaokubaliana na maisha ya chini na yasiyo na hadhi.
Ndio maana watanzania kudai haki ni wavivu sana. Barabara mbovu, umeme unakatwa hovyo, maji ya mgao, hospital huduma za utata, na kadhalika ila wanashinda kuchukua hatua sababu wamefunzwa tokea majumbani kuridhika na kuvumilia kupewa wasichostahiki au kupokea wasichoridhika nacho.
Haya malezi tuachane nayo kizazi chetu kisilee watoto kikabwela.
Mzazi mara moja moja watoe out watoto wako kwenye hotel nzuri. Wananulie zawadi na kuwaambia ni matokeo ya tabia nzuri na adabu zao nzuri.
Kwenye friji mazaga kama juice za kutengeneza nyumbani zisikose. Mkeo ajifunze kutengeneza keki, cookies, bites, awe anawatengenezea watoto. Na mara moja moja unanunua crate au katoni ya soda unaweka kwenye friji madogo wasikae kinyonge wakiona watu wanakunywa huko nje.
Watoto hakikisha wanalalia shuka safi, magodoro yabadulishwe kwa wakati. Na mavazi wawe nadhifu.