Mashaxizo
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 6,707
- 3,346
Ktk kuisaka shahada nimekuwa nikichanganywa na malecturer kutokana utofauti wao wa yale wanayoyafundisha vyuoni!
Hapa nitaweka mifano miwili:
Wadau naamini hilo tatizo halipo kwenye Sheria tu bali hata cozi nyengine lipo!
Jee hili ni kosa la TCU kama wao ni wapitishaji wa mitaala ya vyuo?
Au ni kosa la Malecturer?
Au ni kosa la chuo husika kwa kubadili malecturer?
Tujadili.
Hapa nitaweka mifano miwili:
- Katika Adminstative law, tulifundishwa 'Alter ego theory' tukaambiwa inahusiana na uwajibikaji wa mawaziri! Ikumbukwe, legal system ya Tz ni zao la Common law = tumecopy na kupaste legal sytem ya Uingereza!
Alter ego theory ukiigogle unaletewa mambo mengine kabisa na wala haina mahusiano na administrative law! Bali inaongelea limited liabity ktk makampuni inayoongelea mambo ya hisa!
Mmh! Hiyo kitu iliniumiza kichwa mwisho wa siku nikasema lecturer ndie necta wangu!
Kwa bahati njema, mara hii tunacorse ya "bussiness association law"
Madam ametufundisha sifa za Company na kuelezea zile sifa nilizozikuta gogle kuhusu ile Alter ego theory, nikasema wacha nijaribu kumuuliza, mwee! Hajawahi hata kuisikia ingawa kile alichotufundisha ni Alter ego theory ya Uengereza!
- Katika Land law, tulifundishwa kitu kinaitwa 'Land value' akatupa theory ya Nyerere kuhusu land value, short and clear ni kuwa Nyerere alisema 'Ardhi tupu haina thamani yoyote!' tukaambiwa Nyerere aliitoa hiyo theory mwaka 1958 ili kuzuia ardhi ya Tz isiuzwe kwa wazungu, ili vizazi vijavyo (akina sisi) tupate ardhi! Na hiyo iko wazi na nitofauti na Kenya ambako ukizaliwa na familia isiyo na ardhi hautoweza kupata ardhi kamwe!
Mkanganyiko umekuja semister hii katika cozi 'Conveyancing law' inahusu transfer of land, na mada zake ni zile zile za Land law (Lease, sale na mortgage)
nilianza kujiuliza hapo, hili somo linafaida gani wakati hizo topic tumeshazisoma?
Jee hili ni kosa la chuo husika au TCU?
pili, huyu madam wa sasa naye akaja na mada ya 'land value' kwa vile alijua tumeshasoma, akatuuliza 'mnafahamu nini kuhusu land value?' mimi nikamjibu na kumshuka kama tulivyofundishwa. Afanalek kufa hakuna breki! Huyu Madam hata 'Nyerere theory of land value' haijui, na ukizingatia Nyerere ndie muasisi wa hiyo theory hapa Tz!
Wadau naamini hilo tatizo halipo kwenye Sheria tu bali hata cozi nyengine lipo!
Jee hili ni kosa la TCU kama wao ni wapitishaji wa mitaala ya vyuo?
Au ni kosa la Malecturer?
Au ni kosa la chuo husika kwa kubadili malecturer?
Tujadili.