KERO Wanachuo wa Mwaka wa Kwanza (RADIOLOGY) Chuo cha Nkinga wamekuwa wakilipishwa pesa ambazo washalipa

KERO Wanachuo wa Mwaka wa Kwanza (RADIOLOGY) Chuo cha Nkinga wamekuwa wakilipishwa pesa ambazo washalipa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mmoja wa mzazi wa mwanachuo wa mwaka wa kwanza radiology kutoka Chuo cha Nkinga Health Institutes, Igunga Tabora.

Kumekuwa na gharama zisizo na tija na kuzijurudia, huko nyuma wanafunzi walilipishwa hela ya field sh Laki mbili ambayo unaingiza kwenye account ya chuo baadaye hiyo hela hawakupewa bali walienda field kwa nauli zao na wakajitegemea chakula, mwisho uongozi ukawaambia hiyo hela itatumika kulipia wahusika watakaowafundisha pamoja na clinical coat zenye muhuri wa chuo na field itafanyika kwa mwezi mmoja lakini mwisho field ilifanyika kwa wiki mbili tu.

Wiki hii tena wanachuo wameambiwa walipie elfu 35 kwaajili ya clinical coat yenye mhuri kwaajili ya mtihani, na muda huo tayari ma-clinical coat hayo yenye muhuri wanayo, wanataka mengine tena.

Yaani kila baada ya mwez linakuja lingine linataka gharama, na wanachuo waanambiwa usipolipa hutofanya mtihani.

Hli linaumiza kwetu sisi wazazi!

Kuhusu hizo hela uongozi wa chuo wanasema kuwa zinaenda kulipia ufundishaji huko wanakoenda field pamoja na malipo ya malazi na matumiz ya umeme na maji lakin Kuna wanaobaki chuoni field yao ipo hapo hospital ya nkinga lakn bado wanalipa hiyo sh 200,000.

Kinachoumiza zaidi hela ya field imekuwa lazima kulipwa mpaka kufikia baadhi ya wanachuo walioshindwa kulipa kuzuiliwa kufanya mitihani.

Ada tunayolipa inacover kila kitu maan hatujawahi ambiwa tuchangie hela ya maji au umeme
 
Mzazi una uhakika na maneno ya mwanao kwanza kabla ngazi husika hazijaguswa maana unaweza sema chuo kumbe kijana ana mji wake tayari
 
Hakuna mwanafunzi hapo ndugu mzazi

Ipo siku utaambiwa amepasua amoeba ya chuo na utatakiwa kulipa laki tano
 
Kwanza acha kupeleka mtoto chuo cha kichochoroni ova😎
 
Kumbe cha wapi? Au ni kwasababu cha dini?
Ulitaka vyuo vyote viwe Daslamu na vya GVT!?

Nkinga ni chuo Bora sana kwa elimu na mazingira pia wana Hospitali yenye hadhi ya RRH inayotumika kama Teaching hospital na kwasasa kwakushirikiana na shirika moja la Dini wameanzisha mafunzo ya Uzamili/Ubingwa kwenye Upasuaji kana vile COSECSA inavyoshirikiana na hospitali baadhi kama Bugando kutoa mafunzo ya Ubingwa kwenye Upasuaji

Na wako vizuri zaidi kwenye matibabu pengine kuliko Shy RRH, Tabora RRH, hadi Singida RRH

Sasa unaweza sema hapo ni Uchochoroni!?? Exposure anayopata hapo Mwanafunzi unaweza sema anaesoma City College!?
 
Usinilishe maneno mzee, chuo sio majengo pekee kama hiko kingikua chuo kizuri na hospital unayosema ina faida kwa wanafunzi wasingeenda mafunzo wiki mbili tena kwa taabu na kusingekua na hiyo miyeyusho.
 
Sawa mkuu
 
Back
Top Bottom