Wanadamu tujifunze kuwa wastaarabu

Wanadamu tujifunze kuwa wastaarabu

Kheri ya "Mwaka Mpya"

Jana nilikuwa kwenye manywaji, nikawa nimekaa meza moja na dada ambaye tunafahamiana lakini siyo rafiki yangu.

Akaja kaka mmoja ambaye ananifahamu. Aka "force" kuninunulia bia. Nilimsihi sana kuwa sikuwa nahitaji kunywa kwa muda huo lakini na yeye aliniomba sana "Madam...(huku akitaja jina langu) naomba nikununulie japo bia mbili"

Nikaona isiwe tabu, kwa kuwa nilikaa na yule dada ambaye alikuwa anakunywa Serengeti Lite, basi nikamwambia nitakunywa Serengeti Lite. Akamlipa waitress hela ya bia mbili kiasi cha Tshs. 3,000.

Yule kaka akaenda zake kukaa sehemu nyingine mbali kabisa na pale nilipokuwa nimekaa na huyo dada.

Nikampa yule dada zile bia mbili kwa kuwa mie sikuwa na uhitaji nazo. Dada yule akanishukuru sana.

Dada akanywa bia moja. Sikuamini macho yangu! Yule dada akamuita mhudumu na kumwambia maneno yafuatayo: "Samahani dada, naomba urudishe hii bia moja, halafu unipe hela kiasi cha Tshs.1,500."

Waitress bila hiyana akachukuwa ile bia akairudisha counter, akamletea yule dada hela kiasi cha Tshs.1,500. Yule dada akachukua ile hela akaweka kwenye handbag, akaniaga na kuondoka zake.

Msemo wa wanaJF "Aibu niliona mimi"

Hivi nyie watu mnaoringa na kutamba kuwa nyie ndio kabila kubwa na kabila lenye watu wengi Tanzania, kwanini ustaraabu wenu unakuwa chini kila uchwao? Acheni ushamba wenu huo.
Sijaona tatizo la huyo rafiki yako, kama ambavyo wewe ulikataa kununuliwa bia kwa sababu hukua na uhitaji, ndivyo hivyo hivyo ambavyo naye alikuwa hana kiu ya bia, alikunywa hiyo moja kwa kukuheshimu wewe tu, na hiyo moja iliyobakia, ulitaka aifanye nini ?, ulitaka aimwage ? au ulitaka aiache hapo wahudumu wa baa waichukue waiuze tena ?, aliona bora bora achukue hiyo hela imfae baadae, Na wewe kuwakashifu kabila zima kwa madhaifu ya mtu mmoja huo sio ustaarabu pia
 
Mtoa ofa katoa hela, aliyepewa ofa kagawa ofa, aliyedandia ofa kakubali ofa, kabadili ofa kuwa hela kasepa 😁.. Hicho ni kipaji cha kuishi mjini
 
Sijaona tatizo la huyo dada, huenda kiwango cha idadi bia ambazo huwa anatumia zilikuwa zimefikia. Sasa ulitaka aiache, me naona kama kawivu kamekushika hivi.
 
Hata hivyo kwenye uzi wangu nimesema nilikuwa sijihitaji bia kwa muda huo. hahahaahh
Kwa hiyo ndiyo mnaitana kunishambulia kisa kaswali kadogo chakari mtabari?

Uje nikununulie basi leo.
 
Hapana mkuu unaweza ukaenda kunywa whisk au wine sio lazima beer.

Kuna bar wanaoga kumbe.....asante kwa elimu.
hahahahahahahaahah, JF raha sana. Tumuombe Mungu atujalie tuuone mwaka 2020. hahahah
 
Back
Top Bottom