Kheri ya "Mwaka Mpya"
Jana nilikuwa kwenye manywaji, nikawa nimekaa meza moja na dada ambaye tunafahamiana lakini siyo rafiki yangu.
Akaja kaka mmoja ambaye ananifahamu. Aka "force" kuninunulia bia. Nilimsihi sana kuwa sikuwa nahitaji kunywa kwa muda huo lakini na yeye aliniomba sana "Madam...(huku akitaja jina langu) naomba nikununulie japo bia mbili"
Nikaona isiwe tabu, kwa kuwa nilikaa na yule dada ambaye alikuwa anakunywa Serengeti Lite, basi nikamwambia nitakunywa Serengeti Lite. Akamlipa waitress hela ya bia mbili kiasi cha Tshs. 3,000.
Yule kaka akaenda zake kukaa sehemu nyingine mbali kabisa na pale nilipokuwa nimekaa na huyo dada.
Nikampa yule dada zile bia mbili kwa kuwa mie sikuwa na uhitaji nazo. Dada yule akanishukuru sana.
Dada akanywa bia moja. Sikuamini macho yangu! Yule dada akamuita mhudumu na kumwambia maneno yafuatayo: "Samahani dada, naomba urudishe hii bia moja, halafu unipe hela kiasi cha Tshs.1,500."
Waitress bila hiyana akachukuwa ile bia akairudisha counter, akamletea yule dada hela kiasi cha Tshs.1,500. Yule dada akachukua ile hela akaweka kwenye handbag, akaniaga na kuondoka zake.
Msemo wa wanaJF "Aibu niliona mimi"
Hivi nyie watu mnaoringa na kutamba kuwa nyie ndio kabila kubwa na kabila lenye watu wengi Tanzania, kwanini ustaraabu wenu unakuwa chini kila uchwao? Acheni ushamba wenu huo.