Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Wanadamu katika zama tunazoishi tumefikia hatua inayoweza kuharibu kabisa Dunia tunayoishi na kutowesha kabisa kizazi cha jamii yetu.Leo kutokana na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia mtu mmoja tu anaweza akafanya maamuzi ya kuangamiza na kutisha kabisa.
Kama ni uharibifu wa mazingira binadamu wa leo tumeiharibu siyo Dunia peke yake ila tunajitanua na kuharibu maeneo mengine.
Kiwango mauaji,ubaguzi na ukatili unaofanyika leo ni wa kutisha.Nchi zenye vita na njaa zimeongezeka maradufu hali ya thamani ya utu wa binadamu inazidi kutwezwa katika maeneo mengi Duniani kuliko kipindi chochote kile.
Kuendelea kutafuta suluhisho kwa kurekebisha tunavyoviona nje katika ulimwengu wa vitu ni dhahiri hakutusaidii tena.
Kukata mti na kupanda miti hakutaisaidia misitu yetu kama watu hawatabadili namna wanavyoiona miti katika ulimwengu wao wa kiakili.Kama ni kuratibu vitu vinavyoonekana"ulimwengu wa vitu" watu wameratibu sana lakini shida ni kama inazidi kuimarika.
Pamoja na huduma za Afya na usafi kuboreshwa bado maradhi yameongezeka mara dufu.Pamoja na matumaini makubwa juu ya maendeleo ya sayansi na teknolojia kwenye mfumo mzima wa tiba bado uhai wa binadamu unazidi kuwa mashakani.
Mataifa mengi yamekuwa yakisisitiza umajumui,umoja,amani na tangamano la kitaifa lakini msisitizo huo bado umekuwa kama wimbo unaoudhi.
Wachochezi wa machafuko,wasaliti na wavunjifu wa amani wamekuwa wakisakamwa na wengine kuishia magerezani lakini ni kama wamekuwa wakizaliwa wapya.
Sababu za kuyaingiza mataifa kwenye machafuko zimekuwa zikitafutwa hata kama haipo licha ya amani kuwa jambo la thamani sana katika maisha ya wanadamu.
Dini zimeongezeka na imani zenye itikadi kali " religious extremism" zimeongezeka kwa wingi zaidi tukitegemea ukamilifu lakini tunaona baadhi ya imani hizohizo zikizidi kutumika vibaya.
Familia kama sehemu ya msingi ya uundwaji wa Taifa lolote lile Duniani licha ya msisitizo mkubwa unaotolewa juu ya malezi ya familia bado familia nyingi leo zimeharibika kana kwamba hakuna jitihada zozote zinazochukuliwa kuzinusuru.
Wazazi leo wanatamka laana kila uchao wakiwatazama watoto waliowazaa wenyewe lakini ni kama anazidi kutonesha jeraha.
Ninakiri kushuhudia uwepo wa jitihada nyingi zinazofanywa na mtu mmojammoja,familia mojamoja,serikali,taasisi binafsi mbalimbali katika kurekebisha utu wa Mwanadamu lakoni nipende kusema wazi kabisa kuwa "tumerekebisha sana nje sasa tuingie ndani".