Makonde plateu
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 1,443
- 3,480
Mtanzania Vivian Larsen aliyekuwa akiishi Nchini Denmark ameripotiwa kukutwa akiwa amefariki nyumbani kwake Nchini humo akiwa peke yake nyumbani huku ikiwa haijulikani ni lini umauti umemkuta wakati mume wake yupo safarini kikazi.
Juhudi za kuwasiliana na Polisi nchini kupata taarifa zaidi zimekwama kwa kuwa Polisi bado wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo chake.
Inadaiwa marehemu alikuwa anaishi Nchini Uhispania kabla hajaolewa na mume wake Brian Larsen mnamo mwaka 2016. Marehemu ana ndugu ambaye ni pacha wake anayeitwa Viola ambaye anaishi Mikocheni Dar es Salaam Tanzania.
Kama kuna Mtanzania yeyote aliyekuwa karibu na marehemu au kufahamiana naye enzi za uhai wake anaombwa kutoa ushirikiano wake, na familia ingefarijika sana.
Marehemu ana mtu mmoja wa familia alieoana na binamu yake Vivian anayeishi Denmark lakini naye alikuwa hajui kama Vivian yuko Denmark - Copenhagen. Taarifa alizokuwa anajua ni kwamba Vivian alikuwa anaishi Uhispania kama Mwanamitindo kwahiyo na yeye yuko kwenye masikitiko na mshangao wa kifo chake.