Wanafunzi 11,413 hawajaripoti Kidato cha Kwanza Rukwa

Wanafunzi 11,413 hawajaripoti Kidato cha Kwanza Rukwa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wanafunzi 11,413 ambao ni asilimia 45 ya wanafunzi 25,362 waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule wa sekondari mkoani hapa hawajaripoti shuleni tangu shule hizo zilipofunguliwa Januari 9 mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Queen Sendiga amesema hayo Februari 2, 2023 wakati akitoa maelekezo kwa wakuu wapya wa wilaya katika wilaya za Sumbawanga na Kalambo.

Wakuu hao wa wilaya walioapishwa ni Dk Jane Nyamsenda ambaye atahudumu Wilaya ya Sumbawanga na Lazaro Komba aliyeenda Wilaya ya Kalambo.

Kufuatia kundi kubwa la wanafunzi kutokuripoti shuleni ameagiza kufanyika kwa masako wa nyumba hadi nyumba ili kuwabaini watoto ambao hawajaripoti shuleni ili waanze kwenda shule haraka iwezekanavyo.

Aidha, amewataka wakuu hao wa wilaya kushughulikia changamoto ya ukosefu wa madawati katika shule za msingi ambapo wanafunzi wanakaa sakafuni kutokana na kukosekana kwa madawati 13,458.

"Nindeni mkashughulikie changamoto ya madawati ambapo wilaya ya Kalambo tunahitaji madawati 1,209, Sumbawanga 4,649 na Nkasi ni 7,600 ifikapo Februari 28 sitaki kusikia wala kuona watoto wanakaa chini," amesema.

Pia amewataka kusimamia miradi ya maendeleo, ikiwemo kuhakikisha miradi yote iliyoibuliwa wananchi ikiwemo zanahati na vituo vya afya inakamilika.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dk Jane Nyamsande amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa uteuzi wake huku akiahidi kufanya kazi kwa weledi na maarifa ili kufanikisha lengo la Serikali kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Naye, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Silafu Maufi amewataka wateule hao wa Rais kufanya kazi kwa ushirikiano ili waweze kuwaletea wananchi maendeleo kwenye maeneo wanayokwenda kuyaoongoza.

MWANANCHI
 

Attachments

  • 1675409315662.png
    1675409315662.png
    83.9 KB · Views: 4
Shule kufanya nini wakati ndugu zao wamesoma na wamemaliza vyuo na wamerudi nyumbani kuchoma mkaa?

Wazazi wameelevuka sana sahivi, hawasemi lakini kwa matendo wanaongea. Taifa linaangamia kwa kukosa viongozi makini na wenye upendo

R.I.P JPM
 
Huo ni mkoa mmoja tu, unganisha nchi nzima utapata wanafunzi wengi. Ishu kubwa iko hivi, elimu imekuwa ni ya kujua kusoma na kuandika tu. Elimu ya sekondari imekuwa haina mvuto sana kwa sababu vijana wengi huishia kupoteza muda mwingi shuleni na mwisho anarudi mtaani kuparangana na mishe za mitaani. Vijana wanaona wenzao wanamiliki fedha nyingi wangali wadogo bila mishahara, wanaendesha bajaaj na bodaboda, wamejenga, kuna wengine wanamiliki studio za kurusha nyimbo na season kwenye simu na flash, sasa kijana anakosa focus ya elimu mbeleni itakuaje, anaona haina maana kwenda sekondari kupoteza muda wakati anaweza kupata fedha nyingi hata bila hiyo elimu ya sekondari flat
 
Back
Top Bottom