Wanafunzi 112 chuo cha VETA Geita wanufaika na kusoma bure

Wanafunzi 112 chuo cha VETA Geita wanufaika na kusoma bure

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Wanafunzi wa chuo cha VETA Geita kilichopo kata ya Buhalahala katika halmashauri ya manispaa ya Geita wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusogeza huduma ya masomo bure katika chuo hicho.

Wakizungumza na Storm FM baadhi ya wanafunzi wamepongeza hatua hiyo huku Mkuu wa chuo cha VETA Geita Bw. Thadeus Panga akieleza kuwa jumla ya wanafunzi waliopo ni 112 kati ya hao wanaosomea ufundi wa umeme ni 13, wanaosomea upishi ni 68, wanaosomea ufundi bomba ni 31.

Mwenyekiti Wanawake na Samia mkoa wa Geita Bi. Adelina Kabakama akiwa katika chuo hicho ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi wa Geita kutumia fursa ya kusoma bure katika chuo hicho ili waweze kujikwamua kiuchumi.
 
Back
Top Bottom