Wanafunzi 17 wafikishwa mahakamani kwa tuhuma za ulaghai wa mikopo HESLB

Wanafunzi 17 wafikishwa mahakamani kwa tuhuma za ulaghai wa mikopo HESLB

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa onyo kali kwa waombaji wa mikopo, ikisisitiza kuwa haitavumilia vitendo vya kughushi nyaraka kwa lengo la kujipatia mikopo isivyo halali.

Onyo hilo limetolewa baada ya wanafunzi 17 pamoja na mhitimu mmoja kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya juu jijini Dar es Salaam kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kughushi nyaraka, kutoa taarifa za uongo na kujipatia mikopo kwa udanganyifu.

Washitakiwa hao wanatoka katika vyuo mbalimbali ikiwemo IFM, CBE, UDSM, NIT, DMI, MNMA, DIT na Chuo Kikuu cha Kairuki.

Mahakama imeelezwa kuwa kati ya Juni 2024 na Novemba 2025, washitakiwa hao walitumia mfumo wa OLAMS kuwasilisha taarifa za uongo, ikiwemo madai ya ulemavu wao au wa wazazi wao ili kupata kipaumbele katika mikopo ya elimu ya juu.

Baadhi yao wanadaiwa kufanikiwa kupata mikopo yenye thamani ya mamilioni ya shilingi kupitia mbinu hizo, ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 9, 2026 kwa ajili ya kusikilizwa kwa hoja za awali.

Soma pia ~ Abdul Nondo: Utoaji mikopo kwa Wanafunzi wa vyuo nchini unafanyika kwa ubaguzi sana
 
Serikali iache rongo rongo, itoe mikopo kwa watoto wote bila kujali hali zao! Si ni mkopo bwana!
 
Wanafunzi 17 na mhitimu mmoja kutoka vyuo mbalimbali Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kughushi nyaraka, kutoa taarifa za uongo na kujipatia mikopo kwa njia za udanganyifu.

Mahakama imesema kati ya Juni 2024 na Novemba 2025, washitakiwa walitumia mfumo wa OLAMS kuwasilisha taarifa za uongo, ikiwemo madai ya ulemavu wao au wa wazazi wao ili kupata kipaumbele katika mikopo ya elimu ya juu.
 
Ukichunguza vizuri ni vijana wa CHASO..
REFER YULE ALIYEKAMATWA MWANZA KWA UKOPESHAJI
 
Back
Top Bottom