PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo, Jumatano tarehe 29/07/2026 imewaachia huru wanafunzi 18 wa Vyuo Vikuu mbalimbali Nchini wakiongozwa na Frank Benjamin Kayamba waliokuwa wanatuhumiwa kughushi nyaraka mbalimbali ili wanufaike na mikopo inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, kinyume na tararibu
Mahakama kupitia Hakimu Mkazi Mkuu Romuli Mbuya, imefikia uamuzi huo baada ya kukubaliana na mapingamizi yaliyowekwa na Wakili wa utetezi Peter Madeleka aliyeieleza Mahakama kuwa hati ya mashaka inakosa nguvu za kisheria za kuendelea kubaki Mahakamani kutokana na kwamba upande wa Jamhuri haujaambatanisha maelezo ya mashahidi kwenye hati hiyo kama kanuni za msingi zinavyoelekeza
Soma: Wanafunzi 17 wafikishwa mahakamani kwa tuhuma za ulaghai wa mikopo HESLB
Awali akiwa Mahakamani hapo, Wakili wa Serikali Cuthbert Mbilinyi aliieleza Mahakama kuwa kesi hiyo Na. 13088/2026 ambayo upelelezi wake ulikuwa umekamilika imekuja kwaajili ya usikilizwaji wa hoja za awali, na kwamba upande wa Jamhuri ulikuwa umeshakamilisha kuweka kwenye mtandao wa Mahakama taarifa zote hitajika.
Hata hivyo, muda mfupi baada ya Mahakama kuwaachia huru wanafunzi hao, wakiwa wanatoka Mahakamani hapo walikamatwa tena na maafisa wa Jeshi la Polisi, na taarifa tulizonazo ni kwamba wanafunzi hao watapelekwa Kituo cha Polisi cha Kati (Central Police Station) kwaajili ya taratibu nyingine za kisheria, kwa sasa wakiwa wamehifadhiwa kwa muda kwenye mahabusu ya Mahakama
Akizungumzia hilo, Wakili Madeleka amesema kwa sasa anafuatilia kujuwa wateja wake (yaani wanafunzi hao) wamekamatwa kwa kosa lipi, ili ajuwe hatua za kuchukua.
Muda mfupi baadaye, Wakili Madeleka akasema “Walikamatwa wakapelekwa Polisi, wameachiwa kwa dhamana baada ya kutakiwa kujidhamini wenyewe, wameambiwa waripoti keshokutwa (Julai 31, 2026) Makao Makuu ya Upelelezi Kitengo cha Kudhibidi Fedha Haramu.”