Wanafunzi 30 wanachama wa 'Al-Shabaab' wasimamishwa

Wanafunzi 30 wanachama wa 'Al-Shabaab' wasimamishwa

King Kong III

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
56,205
Reaction score
79,515
Mwanafunzi Rajabu wa kidato cha tatu shule ya sekondari mwanalugali,Kibaha,ambae ni member wa kikundi cha al-shabaab na al-qaeda(vyote vikundi vya shuleni kwao) amefukuzwa shule pamoja na wenzake 29 kwa kosa la kumpiga mwalimu na kosa la kuanzisha vikundi shuleni kinyume cha sheria.

Nawasilisha

Wanafunzi thelathini wanaodaiwa kuanzisha vikundi vya Al-Qaeda na Al-Shabaab katika Shule ya Sekondari ya Kata Mwanalugali, iliyopo Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, wamesimamishwa masomo hadi Bodi ya Shule itakapoamua vinginevyo.

Uamuzi huo ulifikiwa jana shuleni hapo katika mkutano wa walimu na wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule hiyo.

Katika mkutano huo, wazazi walishinikiza kwa kauli moja wanafunzi hao kusimamishwa masomo baada ya mmoja wao ambaye ni mwanachama wa kundi mojawapo, Rajab Mohamed, kumpiga na kumvunja jino mwalimu wake Bw.Lazaro Sule.

Wanafunzi waliofukuzwa ni wa kidato cha pili na tatu ambapo wazazi wenye watoto, walikabidhiwa barua za kusimamishwa masomo ili kutoa nafasi ya kufanyika uchunguzi.

Katika uchunguzi huo, wanafunzi ambao itabainika kuwa chanzo cha vurugu shuleni hapo, watachukuliwa hatua zaidi na wale ambao watanusurika, wataruhusiwa kuendelea na masomo.

Miongoni mwa wazazi hao, Bi. Dina Koya, alisema wanafunzi hao wametia doa shule hiyo kwa kufanya vitendo ambavyo haviwezi kuvumilika kwani wanatia hofu hata kwa wananchi wa kawaida.

"Wengine wanajihusisha na vitendo vya uvutaji bangi na hutumia mapanga kufanya vurugu, hii shule tumeijenga wenyewe kwa kutoa eneo na tumebeba vifusi vya udongo, leo hii baadhi ya wanafunzi wanafanya ionekane haina maana, kimsingi hatuwezi kukubali ni heri waondoke, watatuharibia shule yetu," alisema mzazi mwingine Bw.Ally Maandiko.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Aron Ndunguru, alisema lengo la kusimamishwa wanafunzi hao ni kupisha uchunguzi juu ya vikundi hivyo.

Wanafunzi wa kidato cha tatu ambao wanadaiwa kuunda kikundi cha Al-Qaida ni Mandela Ibrahim, Kibabu Majid, Mbaraka Said, Kelvin Michael, Daniel Alfonce, Rajab Mohamed, Makame Shaban, Khalifa Rashid, Mohamed Abdu, Simon John, Pascal Emanuel, Elizabeth Yusuph, Fausta Michael, Zakia Rashid na Sikudhan Juma.

Wengine wanaounda kundi la Al-Shabaab ambao ni wanafunzi wa kidato cha pili ni Shakila Mohamed, Caroline Hillary, Zainab Dokodoko, Issa Jumanne, Abel Nambala, Shaban Rajab, Michael Mhilu, Bafana Suta, Clinton Stanford, John Peter, Shaban Siraji, Nasoro Ally, Raymond Stephen na Maimuna Abel.

via
gazeti la Majira

Source: wavuti
 
Kibaha? The right place 4 the foo...si ipo pwani hii?expect nothing more than religious related issues wether in schools or any where around the place
 
al-shabaab wanafuata sheria za shule daily wanaatend class ila al-qaeda bana wao niwale manunda wanashinda maporini muda wa shule kutoka nawenyewe wanarudi nyumbani.
 
Mwanafunzi Rajabu wa kidato cha tatu shule ya sekondari mwanagati,Kibaha,ambae ni member wa kikundi cha al-shabaab na al-qaeda(vyote vikundi vya shuleni kwao) amefukuzwa shule pamoja na wenzake 29 kwa kosa la kumpiga mwalimu na kosa la kuanzisha vikundi shuleni kinyume cha sheria.

Nawasilisha
sahihisha ni mwanalugali.

kuwafukuza shule si suluhisho - hilo kundi litaendelea kukua ukizingati hao madogo wote ni wazawa wa pale pale kibaha.
 
Huyo mwalimu sasa yupo hatarini maana sasa wamepata nafasi nzuri ya kumfanyizia wakiwa nje ya shule,al shaabab wamekwishaingia mpaka mashuleni na wanasambaza sumu kali.
 
sahihisha ni mwanalugali.

kuwafukuza shule si suluhisho - hilo kundi litaendelea kukua ukizingati hao madogo wote ni wazawa wa pale pale kibaha.

Thanx fuso ngoje ni-edit
 
Hayo majina ya hayo makundi tu yanatosha kuwafuta hao wanafunzi wote wa makundi yote mawili shule wakaanzishie huko mitaani wakahangaike na kina afande kova!!!!!!!ndo maana yanafeli mitihani sbb ya ******
pale school mtu unaenda kwa ada za wazazi wako ,tenaukiwa pekeyako unakuta wadogo/wazazi wamejichanga wee wameuza hadi kashamba kalokuwa kanaisaidia familia .we unaenda pale unakutana na watu usiowafahamu eti mnaungana kwenye mapombe ya kienyeji ,mabangi .af siku ukifurumishwa unaanza kulia ,utapokuta hali ni mbaya zaid dingi ,na mama wanakaribia kufa kwa mawazo kashamba kao wameuza ,asee tunawapa wazazi tabu sana!!!!!!!!!
 
Tupen majina ya hao watoto wengine 29 c tunaongea tu maana hata wakina maimartha wa jesse naye walikuwa na kikundi chao kwa jina hilo kipind fulan kwa ajili ya kusutana
 
Tupen majina ya hao watoto wengine 29 c tunaongea tu maana hata wakina maimartha wa jesse naye walikuwa na kikundi chao kwa jina hilo kipind fulan kwa ajili ya kusutana
Nafikiri majina sio issue, wala jina la kikundi sio issue..

Issue hapa ni moja tu, je kikundi/vikundi hivyo vilikuwa na lengo gani?
Obviosly, kama walimpiga mwalimu, labda goal ya vikundi hivyo sio nzuri.

mimi nafahamu wanafunzi wa shule moja Kibaha, walianzisha kikundi.....wavulana, lakini kikundi hicho kilikuwa kwa ajili ya kupambana na jamaa wa bodaboda ambao walikuwa wanawatongoza wasichana wa shule, kuwatia mimba na mara nyingi vijana hao waliwakimbia wasichana hao.
kaka zao wakaona huu ni ******, hakuna ruhusa ya kijana wa boodaboda kusogelea dada zao wanaosoma, wakawa wanarudi nao kwa makundi kutoka shule, na wakawa wanaondoka majumbani mwao kwa wakati na kukutana kuelekea shule....

kama mwanaharakati wa elimu...........this was a good kikundi, hata kama wangekamata kijana mmoja wa bodaboda wakamtwanga sawasawa, i would have supported them with passion.
 
..students deserve warning before firing them..

u seem to know how to deal with misbehaving students than their own teachers.
Kaanzishe shule yako halafu uwe unatoa onyo tu kwa wanafunzi wanaong'oa watu meno uone kama hamtabaki vibogoyo!
 
u seem to know how to deal with misbehaving students than their own teachers.
Kaanzishe shule yako halafu uwe unatoa onyo tu kwa wanafunzi wanaong'oa watu meno uone kama hamtabaki vibogoyo!

i think the proper way is to suspend all student who was involved
 
u seem to know how to deal with misbehaving students than their own teachers.
Kaanzishe shule yako halafu uwe unatoa onyo tu kwa wanafunzi wanaong'oa watu meno uone kama hamtabaki vibogoyo!

Lol! spot on !!:lol:
 
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Aron Ndunguru, alisema lengo la kusimamishwa wanafunzi hao ni kupisha uchunguzi juu ya vikundi hivyo.

Wanafunzi wa kidato cha tatu ambao wanadaiwa kuunda kikundi cha Al-Qaida ni Mandela Ibrahim, Kibabu Majid, Mbaraka Said, Kelvin Michael, Daniel Alfonce, Rajab Mohamed, Makame Shaban, Khalifa Rashid, Mohamed Abdu, Simon John, Pascal Emanuel, Elizabeth Yusuph, Fausta Michael, Zakia Rashid na Sikudhan Juma.

Wengine wanaounda kundi la Al-Shabaab ambao ni wanafunzi wa kidato cha pili ni Shakila Mohamed, Caroline Hillary, Zainab Dokodoko, Issa Jumanne, Abel Nambala, Shaban Rajab, Michael Mhilu, Bafana Suta, Clinton Stanford, John Peter, Shaban Siraji, Nasoro Ally, Raymond Stephen na Maimuna Abel.
 
[h=2]16 FEBRUARY 2012[/h][h=3][/h]

John Gagarini, Kibaha

WANAFUNZI 30 wanaodaiwa kuanzisha vikundi vya Al-Qaeda na Al-Shabaab katika Shule ya Sekondari ya Kata Mwanalugali, iliyopo Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, wamesimamishwa masomo hadi Bodi ya Shule itakapoamua vinginevyo.

Uamuzi huo ulifikiwa jana shuleni hapo katika mkutano wa walimu na wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule hiyo.

Katika mkutano huo, wazazi walishinikiza kwa kauli moja wanafunzi hao kusimamishwa masomo baada ya mmoja wao ambaye ni mwanachama wa kundi mojawapo, Rajab Mohamed, kumpiga na kumvunja jino mwalimu wake Bw.Lazaro Sule.

Wanafunzi waliofukuzwa ni wa kidato cha pili na tatu ambapo wazazi wenye watoto, walikabidhiwa barua za kusimamishwa masomo ili kutoa nafasi ya kufanyika uchunguzi.

Katika uchunguzi huo, wanafunzi ambao itabainika kuwa chanzo cha vurugu shuleni hapo, watachukuliwa hatua zaidi na wale ambao watanusurika, wataruhusiwa kuendelea na masomo.

Miongoni mwa wazazi hao, Bi. Dina Koya, alisema wanafunzi hao wametia doa shule hiyo kwa kufanya vitendo ambavyo haviwezi kuvumilika kwani wanatia hofu hata kwa wananchi wa kawaida.

“Wengine wanajihusisha na vitendo vya uvutaji bangi na hutumia mapanga kufanya vurugu, hii shule tumeijenga wenyewe kwa kutoa eneo na tumebeba vifusi vya udongo, leo hii baadhi ya wanafunzi wanafanya ionekane haina maana, kimsingi hatuwezi kukubali ni heri waondoke, watatuharibia shule yetu,” alisema mzazi mwingine Bw.Ally Maandiko.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Aron Ndunguru, alisema lengo la kusimamishwa wanafunzi hao ni kupisha uchunguzi juu ya vikundi hivyo.

Wanafunzi wa kidato cha tatu ambao wanadaiwa kuunda kikundi cha Al-Qaida ni Mandela Ibrahim, Kibabu Majid, Mbaraka Said, Kelvin Michael, Daniel Alfonce, Rajab Mohamed, Makame Shaban, Khalifa Rashid, Mohamed Abdu, Simon John, Pascal Emanuel, Elizabeth Yusuph, Fausta Michael, Zakia Rashid na Sikudhan Juma.

Wengine wanaounda kundi la Al-Shabaab ambao ni wanafunzi wa kidato cha pili ni Shakila Mohamed, Caroline Hillary, Zainab Dokodoko, Issa Jumanne, Abel Nambala, Shaban Rajab, Michael Mhilu, Bafana Suta, Clinton Stanford, John Peter, Shaban Siraji, Nasoro Ally, Raymond Stephen na Maimuna Abel.

This is scary...
Wamesimamishwa kwa kosa la kuvuta bangi, kuvuruga hali ya usalama kwa kutumia Panga na kwa kumpiga mwalimu (na kumtoa meno). But did they establish any link with the Extremist groups? Do they have any links? Do they get directions from them etc? Sijaelewa kwa nini wameitwa Al Qaeda au Al Shabaab...
 
RR, wamejiita hivyo, nikiwa primary kulikua na jamaa wanajiita ANC walisimamishwa pia nadhani hairuhusiwi kuwa na hiz radical mischievous groups, hayo majina ndio waliochagua, ni kama mungiki
 
Back
Top Bottom