Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
TAARIFA YA MIKOPO KWA WANAFUNZI WALIOKATA RUFAA
WANAFUNZI 4,676 WAPANGIWA MIKOPO YENYE THAMANI YA TZS 15.5 BILIONI
Mfuko wa Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) umetangaza kukamilika kwa upangaji wa mikopo ya wanafunzi waliokata rufaa kwa mwaka wa masomo 2024/2025. Jumla ya wanafunzi 4,676 wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 15.5 bilioni kupitia rufaa.
Kwa undani zaidi:
• Wanafunzi 4,183 wa mwaka wa kwanza wamepangiwa mikopo ya TZS 13.8 bilioni.
• Wanafunzi 493 wa mwaka wa pili na kuendelea wamepangiwa mikopo ya TZS 1.7 bilioni kupitia rufaa.
Aidha, wanafunzi wengine 3,934 wanaoendelea na masomo yao wamepangiwa mikopo kwa mara ya kwanza yenye thamani ya TZS 12.4 bilioni.
Kwa ujumla, mwaka wa masomo 2024/2025 umeshuhudia jumla ya wanafunzi 86,646 wakipangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 273.46 bilioni, ikiwemo:
• Wanafunzi wa mwaka wa kwanza 79,573.
• Wanafunzi wa mwaka wa pili na kuendelea waliopangiwa mikopo kwa mara ya kwanza 7,073.
Kwa taarifa hii, Bodi ya Mikopo (HESLB) inatangaza kukamilika kwa upangaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2024/2025. Waombaji ambao hawakupata mikopo wanashauriwa kujiandaa kuomba wakati dirisha litakapofunguliwa kwa mwaka wa masomo 2025/2026.