Wanafunzi 521 watoroka shuleni Simiyu, Serikali imetangaza mpango wa dharura

Wanafunzi 521 watoroka shuleni Simiyu, Serikali imetangaza mpango wa dharura

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Jumla ya wanafunzi 521 wa Shule mbalimbali Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wameripotiwa kukimbia masomo kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita hali ambayo imeilazimu Serikali kutangaza mpango wa dharura wa kukabiliana na tatizo hilo.

Ni katika kukabiliana na changamoto ya utoro shuleni, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Lupakisyo Andrea Mjukuu wa Kapange, amelazimika kutangaza operesheni ya kuwasaka na kuwarejesha masomoni wanafunzi 521 wanaodaiwa kususa masomo, ikiwa ni pamoja na wazazi wanaohusika kuwaoza au kuwaozesha kukabiliwa na shinikizo la sheria.

“ Tumeanzisha operesheni ya kuwasaka watoro wote. Awe mtoto wa kike, awe wa kiume lazima asome kwa sababu Taifa hili linamuhitaji sana. Kila mtoto (mtoro) tutamfikia kwa jina lake na mahala alipo.Tukikuta mtoto hayupo tutamchukuwa mzazi mpaka atakapotuletea mtoto ndipo tutamuachia, pelekeni salamu,” amesema DC Kapange.

Amesema elimu ni takwa la kisheria na mikataba ya Kimataifa, iliyoridhiwa na Tanzania kupitia Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009, hivyo ni lazima watoto wote waelekee masomoni shuleni kwa faida ya maisha yao na Taifa kwa ujumla

“Elimu ni haki ya mtoto, tunataka mtoto apate haki yake. Yaani wilaya nzima watoto 521 (watoro shuleni) wilaya nzima, hii haikubaliki. Na hii ninayozungumza ni kutoka tarehe 1 mwezi wa 7 mpaka tarehe 12 mwezi wa 9, yaani hapa katikati watoto hawaonekani (shuleni) mnataka kuwapekela wapi! Watoto pingeni kuolewa,” amesema DC Kapange.

“Tunakuahidi tutafanyakazi kwa ushirikiano kwa sababu wewe unaendelea kutupa ushirikiano mkubwa tunapokuwa na changamoto. Kwa hiyo, tunakuahidi kwamba sisi tunakwenda kufanyakazi,” amesema Isabela.

“Tunajua kuna idadi kubwa sna kule (mgodini) wameacha shule wapo mgodini wanafanyakazi. Lakini, tuna changamoto ya wazazi. Hali duni wazazi wanawazuia watoto kuja shuleni ili wakafanye shughuli za kiuchumi,” amesema Mecklina.

Wakati hayo yakijiri, Mkuu wa Wilaya hii ya Bariadi, Lupakisyo Andrea Mjukuu wa Kapange, amelazimika kufunga safari hadi nyumbani kwa mwanamama mmoja mkazi wa Kata ya Dutwa, anayedaiwa kumzuia mwanaye kwenda shuleni na amemuamuru kumpeleka mtoto huyo masomoni, vinginevyo atakiona cha mtemakuni

“Alikuwa anasoma na alikuwa anafaulu mitihani yake yote na mitihani yake yote ninayo, anafanya vizuri (masomoni). Kama umemjenga kichwani kwamba nenda shuleni maadamu wanalazimisha kwanda shule ukafeli, akifeli (mitihani) nakuweka ndani,” DC Kapange ameonya.



Chanzo: EATV
 
Huu utakua ni upuuzi..yani familia imejaa umasikini njaa..hakuna hela halafu kwajirani kuna kubeba tofari unapata buku 10 kwa siku au aende shule akale mboko stress na njaa akirudi home napo njaa..hata angekua huyo dc angacha shule.

Mazingira ya vijijini serikali itoe chakula..hayo maindi yaliyojazwa kwenye maghala yatumike pia kulisha wanafunzi ili wabaki shuleni.

N.b siungi mkono utoro.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
kuna watoto ni 0.0% kichwani hata usomeshe vipi haelewi kitu
Mazingira ndo yanachangia, huko vijijini wanaongea kikabila na shule anasoma kiswahili na mzazi hajui kusoma hata jina lake Sasa hapo mtoto kuwa kilaza wa 0.0 ni mazingira yanakuwa yamechangia, kikubwa huyo mkuu wa wilaya afanye mazingira ya shule yawavutie wanafunzi hasa uji na chakula cha mchana.
 
Huku vijijini Kuna njaa ya hatari usione watu wapo wananyweshana juisi kwenye glasi, watoto wanasshinda kutafuta mabaki ya viazi mashambani!
Inasikitisha sana, ikitokea hao watoto wamekuwa kidogo wanakimbilia mjini wakizani mahitaji yanapatikana Bure tu wakizidiwa na njaa wanaanza kuomba watu baki wawainue kiuchumi kama yatima, serikali iweke nguvu kubwa vijijini kuwawajibisha wazazi wajue kuzaa ni kulea kiumbe mpaka kiwe na uwezo wa kujitegemea kiuchumi, wazazi wa vijijini wamejisahau sana hata viboko wachapwe na kufungwa juu Ili waone umuhimu wa elimu kwa watoto.
 
Kipindi niko mdogo kama ningekuwa najitambua na kujielewa hata mimi ningetoroka na kwenda kusomea taaluma ai ujuzi wowote ule, hizi shile za kukariri Kanuni za voltage na current ni mtego wa kikoloni
 
Mtoto anatoroka anakwenda kupiga mitkas sehemu anajipatia 100 zake
Akiangalia familia yake ngoma nagwa
Mambo magumu!

Ova
 
Back
Top Bottom