Wanafunzi 572,338 kuanza Mtihani wa Kidato cha 4 leo

Wanafunzi 572,338 kuanza Mtihani wa Kidato cha 4 leo

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), kati ya Watahiniwa hao, 543,386 ni Wanafunzi wa Shule ambapo Wavulana ni 250,237 (46.05%) na Wasichana ni 293,149 (53.95%)

Watainiwa ambao ni Wanafunzi wa Shule wenye Mahitaji Maalum ni 614 ambapo 283 ni wana Uoni Hafifu, 24 ni Hawaoni Kabisa, 135 wana Ulemavu wa Kusikia, 11 wana Matatizo ya Mfumo wa Akili na 161 ni wana Ulemavu wa Viungo vya Mwili.

Kwa upande wa Watahiniwa wa Kujitegemea ni 28,952 ambapo Wavulana ni 11,867 (40.99%) na Wasichana ni 17,085 (59.01%). Idadi ya Shule zinazofanya Mtihani ni 5,371 na Vituo vya Watahiniwa wa kujitegemea ni 1,798

Idadi ya Watahiniwa wa Shule ina ongezeko la 1.61% kutoka Idadi ya Wanafunzi 534,753 waliosajiliwa kufanya Mtihani huo mwaka 2022.
 
500k wanamaliza F4? Mbona ni idadi kubwa sana.

Hivi kila mwaka vyuo vikuu vinazalisha graduates wangapi?

Kila la heri kwao.
Ni idadi kubwa ila wataopata C tatu hawatazidi 250k wengi hupata Four na wachache 1-3 na chuo kikuu hufika 80-100k

Unaweza kuangalia hata wewe mliosoma darasa moja Hadi form Four je chuo kikuu mliingia waangapi?
 
Muhimu matokeo yatokayotoka yawe sahihi kadri ya uwezo wao km ilivyokuwa zamani. Sasa hivi mwanafunzi anafaulu anapata FIVISION ONE anaejiunga kidato Cha TANO Ila kichwani ni Tia maji tia maji tu, akibahatika kupata division 2/3 na kwenda chuo kikuu huko ndo uhalisia wa uwezo mdogo hudhihirika zaidi. Yani elimu ya sasa yataka moyo kwa waajiri.
 
Kila la heri Watoto wetu,Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi kwenye mitihani yenu
 
KILA LA KHERI FORM FOUR

Comrade Ally Maftah

  • Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam
  • Mjumbe Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam
  • Mwanzilishi na Mmiliki wa CAM STORE
Anawatakia Kheri wanafunzi wote wa Kidato cha nne wanaoanza mitihani yao leo.

UJUMBE WANGU KWENU.

"HAKUNA MKATE MGUMU MBELE YA CHAI, WEWE NDIO MSHINDI UNAYEMTAFUTA, WEWE NDIO MAFANIKIO"
View attachment 2812256
Ila mjumbe hicho ulichovaa ndio nguo za kikamanda au
 
Back
Top Bottom