BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumapili Januari 15, 2023 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msingwa, wanafunzi 354,277 wakiwemo wenye ulemavu 697, ndiyo walioripoti hadi sasa kati ya wanafunzi 1,070,941 wanaotarajiwa kuingia kidato cha kwanza sawa na asilimia 33 ya matarajio.
Aidha amesema watoto walioandishwa kwa aajili ya kuanza darasa la kwanza ni 1,446,067 wakiwemo wenye ulemavu 2,942 sawa na asilimia 88.48 ya matarajio ya watoto 1,634,365.
Msigwa ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kwenda sekondari wanaripoti shuleni.
Amesema Serikali inagharamia elimu ya msingi na Sekondari kwa kutoa Sh 29 bilioni kila mwezi sambamba na kutoa maelekezo mahususi juu ya michango kwa wanafunzi wanaoingia shuleni lengo likiwa ni kuondoa vikwazo vya wanafunzi kujiunga na shule.
Vilevile amesema jumlanya wanafunzi 14,581 wameandikishwa katika Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Walioikosa (MEMKWA) na kati ya hao 334 ni wenye mahitaji maalum.
MWANAHALISI ONLINE