Wanafunzi 8 wa MUST mbaroni kwa kuwafanyia wengine mtihani

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Wanafunzi nane wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika mtihani wa Electrical Installation Level III unaosimamiwa na NACTVET ambapo waliingia kwenye chumba cha mtihani na kuwafanyia mtihani huo wanafunzi wengine kabla ya kubainika na Msimamizi Mkuu wa kituo.

Taarifa ya leo Oktoba 30, 2026 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya imeeleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa mnamo Oktoba 27, 2026 katika Chuo cha Ufundi Morovian jijini Mbeya baada ya kubainika kuwa picha kwenye barua zao hazifanani na mfumo, huku wakidaiwa kulipwa Shilingi 100,000 kila mmoja.

Katika matukio hayo waliokamatwa ni pamoja na Rashid Mkwandam (mkazi wa Ikuti) aliyemfanyia Shaziri Bakari; Daniel Zacharia (mkazi wa Lupeta) aliyemfanyia Erasto Ng’holo; Rhino Bikura (mkazi wa Iyunga) aliyemfanyia Nehemia Tukonge na Jilala Mathias (mkazi wa Inyala) aliyemfanyia Felix Shibanda

Wengine ni Isack Kasiri (mkazi wa Iyunga) aliyemfanyia Jeremia Sanga; Andrew Ngewe (mkazi wa Inyala) aliyemfanyia Benard Mgala; Marine Chembea (mkazi wa Ikuti) aliyemfanyia Hamisi Mwenga na James Masanja (mkazi van Inyala) aliyemfanyia Leonard Mgala.

Chanzo : Mualid kitenge tv
 
Hivi kwa nini mtu usifanye mtihani wako mwenyewe kuepusha mambo kama haya. Kama unajua mambo huyawezi ulichagua kusoma ili iweje?
 
Wanachuo wanaelewa, kuna muda unashikwa na somo kuanzia 1st year Hadi third year Kila ukufanya hupindui unaona liwalo na liwe bora abet.

Hii ndio maana ya chuo, lazima maajabu yawe yanatokea ili first year wakija wasimuliwe
 
Wanafunzi nane wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika mtihani wa Electrical Installation Level III unaosimamiwa na NACTVET ambapo waliingia kwenye chumba cha mtihani na kuwafanyia mtihani huo wanafunzi wengine kabla ya kubainika na Msimamizi Mkuu wa kituo.

Taarifa ya leo Oktoba 30, 2026 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya imeeleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa mnamo Oktoba 27, 2026 katika Chuo cha Ufundi Morovian jijini Mbeya baada ya kubainika kuwa picha kwenye barua zao hazifanani na mfumo, huku wakidaiwa kulipwa Shilingi 100,000 kila mmoja.

Katika matukio hayo waliokamatwa ni pamoja na Rashid Mkwandam (mkazi wa Ikuti) aliyemfanyia Shaziri Bakari; Daniel Zacharia (mkazi wa Lupeta) aliyemfanyia Erasto Ng'holo; Rhino Bikura (mkazi wa Iyunga) aliyemfanyia Nehemia Tukonge na Jilala Mathias (mkazi wa Inyala) aliyemfanyia Felix Shibanda

Wengine ni Isack Kasiri (mkazi wa Iyunga) aliyemfanyia Jeremia Sanga; Andrew Ngewe (mkazi wa Inyala) aliyemfanyia Benard Mgala; Marine Chembea (mkazi wa Ikuti) aliyemfanyia Hamisi Mwenga na James Masanja (mkazi van Inyala) aliyemfanyia Leonard Mgala.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba watuhumiwa wote wanaendelea kufanyiwa uchunguzi kufuatia vitendo hivyo vinavyokiuka taratibu za elimu.
 
Kwanza kwanini ufanyiwe mtihani? Ndio madhara ya kufaulisha vilaza, watoto ni weupe kichwani, afu ni fundi michundo hao, daaah hasara tupu.
 
Wanafunzi nane wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika mtihani wa Electrical Installation Level III unaosimamiwa na NACTVET ambapo waliingia kwenye chumba cha mtihani na kuwafanyia mtihani huo wanafunzi wengine kabla ya kubainika na Msimamizi Mkuu wa kituo.

Taarifa ya leo Oktoba 30, 2026 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya imeeleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa mnamo Oktoba 27, 2026 katika Chuo cha Ufundi Morovian jijini Mbeya baada ya kubainika kuwa picha kwenye barua zao hazifanani na mfumo, huku wakidaiwa kulipwa Shilingi 100,000 kila mmoja.

Katika matukio hayo waliokamatwa ni pamoja na Rashid Mkwandam (mkazi wa Ikuti) aliyemfanyia Shaziri Bakari; Daniel Zacharia (mkazi wa Lupeta) aliyemfanyia Erasto Ng’holo; Rhino Bikura (mkazi wa Iyunga) aliyemfanyia Nehemia Tukonge na Jilala Mathias (mkazi wa Inyala) aliyemfanyia Felix Shibanda

Wengine ni Isack Kasiri (mkazi wa Iyunga) aliyemfanyia Jeremia Sanga; Andrew Ngewe (mkazi wa Inyala) aliyemfanyia Benard Mgala; Marine Chembea (mkazi wa Ikuti) aliyemfanyia Hamisi Mwenga na James Masanja (mkazi van Inyala) aliyemfanyia Leonard Mgala.

Chanzo : Mualid kitenge tv
Nimefarijika kuona katika hiyo list hakuna jina la Mwanamke aliyefanyiwa mtihani.
 
Hivi kwa nini mtu usifanye mtihani wako mwenyewe kuepusha mambo kama haya. Kama unajua mambo huyawezi ulichagua kusoma ili iweje?
Hii ni culture ya Tanzania, i am afraid to say. Siyo kwenye mitihani tu, ni karibu kila sehemu watu hawako honest. By the way, kama rais wa nchi anaweza kudanganya wazi wazi mchana kweupe kuwa kashinda kwa asilimia 98, huku kila mtu akijua ni uongo, unategemea wananchi anaowaongoza wafanya nini?
 
Kwanza kwanini ufanyiwe mtihani? Ndio madhara ya kufaulisha vilaza, watoto ni weupe kichwani, afu ni fundi michundo hao, daaah hasara tupu.
Hii ndiyo ile mitihani tuliyoita ya trade test zamani?
Tuliita mitihani ya veta kabla ya kuundwa NACTVET?
 
Back
Top Bottom