Wanafunzi tisa wa Shule ya Wasichana ya Utumishi Girls Academy katika Kaunti ya Nakuru wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka 16 ya mauaji kila mmoja kufuatia mkasa wa moto uliosababisha vifo vya wanafunzi 16 mnamo Mei 28, 2026.
Uamuzi huo umeidhinishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) baada ya kupitia ushahidi uliowasilishwa na maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI). Kwa mujibu wa Ofisi ya DPP, uchunguzi wa kina wa ushahidi uliokusanywa ulionyesha kuwa kuna msingi wa kufungua mashtaka dhidi ya washukiwa hao.
Moto huo ulizuka katika bweni la shule usiku wa kuamkia Mei 29 na kusababisha vifo vya wanafunzi 16 pamoja na uharibifu mkubwa wa mali ya shule. Wachunguzi wanadai kuwa mpango wa kutekeleza kitendo hicho ulipangwa saa chache kabla ya moto kuwashwa.
Awali, Mahakama ya Naivasha iliwaruhusu waendesha mashtaka kuwazuilia wanafunzi hao kwa siku 21 ili kukamilisha uchunguzi, ikiwemo uchambuzi wa DNA, uchunguzi wa kisayansi na mapitio ya kamera za usalama (CCTV).
Kwa mujibu wa DCI, picha za CCTV na ushahidi wa kitaalamu zilionyesha mienendo ya baadhi ya washukiwa kabla ya moto huo kuzuka. Wachunguzi pia walidai kuwa vifaa kama vile viberiti, magodoro na mafuta ya taa vilihusishwa na tukio hilo.
Ofisi ya DPP imeeleza wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa visa vya uchomaji moto na vitendo vingine vya uhalifu katika taasisi za elimu nchini. Aidha, imeonya kuwa yeyote atakayepatikana na hatia ya makosa kama hayo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
DPP pia imetoa rambirambi kwa familia za wanafunzi waliopoteza maisha, marafiki zao na jamii ya shule kwa ujumla, huku ikisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha haki inatendeka kupitia mchakato wa mashtaka unaozingatia ushahidi, usawa na sheria.
Kesi hiyo imeendelea kuvuta hisia za Wakenya wengi huku ikizua mjadala kuhusu usalama wa shule, ustawi wa wanafunzi na namna ya kushughulikia migogoro ndani ya taasisi za elimu.
Soma pia Video za CCTV zimefichua wanafunzi nane waliohusika na kuwasha moto bwenini uliosababisha vifo vya wanafunzi 16
Source: Thestar.co.ke