Wanafunzi Ardhi University waandamana kupinga kuzuiwa kuvaa nguo fupi, kubana

Kwa hiyo, je hii habari ya udaku? Au niamini Nipashe ni kama Sani, Ijumaa n.k

naona nipashe imeanza udaku,nilikuwepo chuoni sijaona hayo maandamano..nimeuliza watu wengine wanadai halikuwa tangazo ila makala za wanaharakati na hakuna aliyeandamana.Katika nchi hii kuna vitu vingi vya msingi vya kuandika kwenye magazeti lakini sio minor thngs tena vya kukuzwa kama hiki.ts nonesence kwa gazeti kama nipashe!!!!
 
nna mashaka na hiyo source, and if its true tunaelekea kubaya kwa kweli Nipashe= umbea na udaku (where is the pride of nipashe tulia tukupashe) au sasa slogan ni Nipashe tulia tukupe udaku?, ma-reporter wa sasa bwana
 
Ni bora tungeondoa uhuru wa Mavazi kwenye hii Nchi, kwani hali ni mbaya sana!! Hawa dadaz kwa sasa ni balaa, hata kama ana miguu iliyopinda kama ya Mbwa wa Parokiani naye utamkuta na mavazi ya ajabu kweeeelii!!!
 
kweli apo kutakua na elimu?baadala ya kuandama kwa vitu vyenye msingi wao wanaandama kisa mavazi....hawana lolote wanataka tu kufanya umaeurop
 
hivi vyuo vyetu, kuna siku vitageuzwa mabanda ya kufugia kuku
 
Kuna mambo mawili hapa kama ni kweli manake inaonekana ni uzushi. Kwanza vyuo kazi yake ni utafiti na kufundisha. Kuamua mavazi ya wanafunzi sio kipaumbele chao na nitashangaa chuo kitakachoshindwa kujua adhari za kutokutoa ugunduzi kwa muda mrefu. Pili ni matokeo ya mfumo wa elimu kama shule ipo well demand mwanafunzi ama hana muda wa kujipamba au hana muda wa kuangalia waliojipamba maisha yangeendelea. Ni sawa na zamani baadhi ya walimu wa primary walikuwa wanachapa darasa zima au monigof kuandika majina ya wapiga kelele wakati tatizo halikuwa wanafunzi bali mwalimu hakuwapo darasani.
 
Nilishapiga marufuku kwenye kipindi changu hakuna mini skirt wala vitopu hapo ARU.ambae hawezi akasome kwao. Not in my life time at ARU. LMV ,Pfm'Refi na Baf wanajua hilo.
 
Jaman m npo hapa chuo cha ardhi, sijaliona TANGAZO, KWA HL GAZET LA NIPASHE WAMEANZA KUANDKA UDAKU.

uliza lilipo hilo tangazo kwa wenzako,ndo useme kuwa NIPASHE limeandika udaku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…